TAASISI ZA HAKI ZA BINADAMU ZATAKIWA KUZINGATIA MISINGI YA HAKI.


Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM

Imeelezwa kuwa Taasisi za haki za Binadamu zikizingatia misingi ya kikatiba na kisheria na haki za binadamu zitasaidia kulinda haki hizo na kuondoa changamoto kwa jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa wakati akizungumza katika Mkutano na mafunzo ya siku tatu inayohusisha Mtandao wa Taasisi za haki za Binadamu Afrika wakijadili azimio la Marakeshi ambalo limeweka utaratibu mzuri wa kulinda haki za binadamu.

Olengurumwa amesema kwa mujibu wa katiba na sheria za kimataifa mwenye jukumu la kulinda haki za binadamu ni serikali pamoja na taasisi zake zikiwemo Mahakama pamoja na Polisi.

‘Tunafahamu kwamba ulinzi wa haki za binadamu  mwenye jukumu la kwanza la kulinda haki hizo kwa mujibu wa katiba na sheria za kimataifa ni serikali zetu na taasisi zake na ndio maana tuna polisi’amesema Olengurumwa

Aidha Mratibu huyo amesema ni vyema haki za binadamu zikaendelea kuheshimiwa ili ziweze kusaidia kuitetea jamii katika changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Mohamed Hamis Hamad amesema ili kuzilinda haki za binadamu pasavyo ni vyema taasisi za kiserikali zikatumia nafasi zao katika kuzisimamia ipasavyo haki hizo.

‘Ukizungumza Haki za binadamu unazungumza kusishi katika mazingira mazuri,Afya,Kuishi,Chakula hivyo ukikivunja kimoja kinakuplekea katika mazingira mengine kwa hivyto kwa misingi hiyo kuna haja ya kuimarisha juhudi za pamoja baina ya serikali na wadau wote wa haki za binadamu’.amesema Mohamed

Hata hivyo Mohamed amesema serikali kwa kushirikiana na taasisi za haki za bindamu ni vyema zikatoa elimu kwa jamii kuhusu kuzifahamu haki zao ili kuweza kukuza na kuendeleza haki hizo.

0/Post a Comment/Comments