TAKUKURU ILALA KUENDELEA KUDHIBITI MIANYA YA RUSHWA.

                     Mkuu wa Takukuru Ilala Christopha Myava

                           NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ilala jijini Dar es salaam imesisitiza kuendelea kutilia mkazo wa kudhibiti mianya ya Rushwa kwenye miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu,Maji,Ujenzi na miundombinu katika miezi mitatu ijayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es salaam Mkuu wa Takukuru Ilala Christopha Myava amesema lengo lao ni kudhibiti vitendo vya Rushwa ilikuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi na inakamilika kwa wakati uliopangwa.

Myava amesema watahakikisha miradi yote inayotekelezwa katika jiji la Dar es salaam wanaifuatili kwa lengo la kuziba mapema mianya ya Rushwa kabla upotevu wa fedha haujatokea ili iendane na  thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

Aidha Mkuu huyo wa TAKUKURU ametoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaotumia jina la kuwa maafisa wa taasisi hiyo kwa kuwadai watu pesa, kuwa watachukuliwa hatua kali ili kukomesha vitendo hivyo.

Awali Myava ametoa tahmini ya miezi mitatu iliyopita April mpaka Juni mwaka huu ambapo,amesema TAKUKURU wameweza kuokoa Shiling i Mill.123 na elfu 50 ambazo zimedhibitiwa kutoka kwa watuhumiwa kujipatia fedha hizo kinyume na sheria.

Hata hivyo Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala amewataka wananchi wa mkoa huo kuendelea kuonyesha ushirikiano wa taasisi hiyo kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa pindi wanapozibaini katika maeneo yao.

0/Post a Comment/Comments