TALIBANI WANAPATA WAPI FEDHA ZA KUJISIMAMIA?

 




Kundi hili la wapiganaji linapata pesa nyingi kupitia wadau wao mbalimbali.


Cesar Gudes ambaye ni mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (U.N.) aliyekuwa akifanya kazi Kabul aliwahi kunukuliwa akiliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa kuna biashara ya magendo ambayo inaingiza fedha nyingi kwa wapiganaji hao:


Alisema kuwa Taliban pia wana vyanzo vya ziada vya mapato ambavyo ni pamoja na madini, ushuru na michango. Inadhaniwa kuwa nchi nyingine pia hulifadhili kundi la Taliban kifedha.


Guido Steinberg, kutoka Taasisi ya Ujerumani ya Masuala ya Kimataifa na Usalama (SWP), aliliambia Shirikila la Habari la Ujerumani la DW kuwa:  


"Taliban wana washirika wawili, mmoja ni mshirika asiyeonekana, Iran. Mshirika wao wa pili na muhimu zaidi ni Pakistan."


Kundi la Taliban liliibuka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Afghanistan ambavyo vilifuata kujiondoa kwa Umoja wa Kisovieti nchini humo na kundi hilo lilianzishwa rasmi mnamo 1994.


Wapiganaji wake wengi hapo awali walipigana dhidi ya vikosi vya Kisoviet vilivyokuwa vikidhibiti eneo hilo jaribio ambalo liliungwa mkono kwa siri na Shirika la ujasusi la Marekani CIA. 



#TimesFMDigital 

0/Post a Comment/Comments