TCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI SHAHADA YA KWANZA MWAKA WA MASOMO 2021/2022

 

Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam akia taarifa ya kukamilika kwa awamu ya Kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahiliwa shahada ya Kwanza kwa mwaka was masomo 2021/2022 

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM 

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeendela kuwataka Wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakala au washauri wanaodai wanatoa huduma ya jinsi ya kujiunga na Vyuo vya Elimu ya juu hapa nchini. 

Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam kufuatia kutolewa taarifa ya kukamilika kwa awamu ya Kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahiliwa shahada ya Kwanza kwa mwaka was masomo 2021/2022. 

Akizungumza na wanahabari Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa amewahimiza waombaji waliodahiliwa katika Chuo zaidi ya kimoja kuthihitisha udahiliwa wao katika Chuo kimoja kuanzia Kesho Agosti 24 mpaka Septemba 6 mwaka huu. 

Profesa Kihampa amesema kuwa kwa wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili wa Vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya Siri ili kuweza kujithibitisha katika Chuo husika. 

Aidha Katibu huyo Mtendaji wa TCU amesema kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa mwaka 2021/2022 tume hiyo inatangaza kuwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo itaanza rasmi Kesho Agosti 24 mpaka Septemba 6 mwaka huu. 

"Tume inasisitiza kuwa kwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye Vyuo wanavyovipenda"amesema Profesa Kihampa

Awali akieleza mafanikio ya udahili Awamu ya Kwanza,Profesa Kihampa amesema Jumla ya waombaji 92,809 wametuma maombi ya kujiunga katika Vyuo 74 vilivyoodhinishwa kudahili na  Programs 724 zimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na Program 686 mwaka 2020/2021. 

"Pia katika awamu ya kwanza ya udahili Jumla ya waombaji 68,019 sawa na asilimia 73.2 ya waombaji wote walioomba udahili tayari wameshapata udahili vyuoni na mwenendo wa Kwanza wa Kipindi Cha miaka minne 2018/2019 Hadi 2021/2022 unaonesha ongezeko kubwa kwa waombaji"amesema Profesa Kihampa

Hata hivyo Tume hiyo imezielekeza Taasisi za Elimu za Juu kutangaza Program ambapo bado zinanafasi katika vyuo vyao.

0/Post a Comment/Comments