TETEMEKO LAUA WATU 304 NA 1,800 WAJERUHIWA

 




Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Haiti,na  kuua karibu watu 304 na kuwajeruhi zaidi ya 1,800.


Tetemeko hilo kubwa lineikumba Haiti, na lina  ukubwa wa 7.2 katika vipimo vya Ritcher - liligonga magharibi mwa nchi hiyo Jumamosi asubuhi, na kuvunja,kuharibu majengo ikiwemo makanisa na hoteli.

Waziri mkuu amesema ulikuwa "uharibifu mkubwa " na kutangaza mwezi mmoja wa hali ya hatari..

Kina cha tetemeko hilo la Jumamosi kilikuwa karibu kilo mita 12 ( maili 7.5) kutoka mji wa Saint-Louis du Sud, uchunguzi wa wanajiolojia wa Marekani (USGS) umesema.

Mtetemeko huo ulisikika katika mji mkuu wa Port-au-Prince uliyo na wakazimwengi, umbali wa kilomita 125, na mataifa jirani.

"Nyumba nyingi ziliharibiwa, watu wamefariki na wengine wako hospitali," Christella Saint Hilaire, ambaye anaishi karibu na kina cha tetemeko hilo, aliiambia shirika la habari la AFP.

Waiziri Mkuu Ariel Henry alisema ameandaa timu ya kufanya kazi ya kutoa misaada.

"Kitu cha muhimu ni kuokoa manusura wengi iwezekanavyo waliokwama kwenye vifusi," alisema.

 "Tumefahamishwa kuwa hospitali zimelemewa na kazi hasa ile ya Les Cayes inayowahudumia wale waliojeruhiwa na watu waliovunjika."

Baadaye Bw Henry alifichua kwamba alisafiri kwa ndege juu ya mji wa Cayes.

Rais Joe Biden ameamuru Marekani ''kuingilia kati mara moja" kusaidia nchi hiyo na kusema kwamba shirika la USAID litasaidia katika juhudi za "kutathmini uharibifu na kuwaokoa wale waliojeruhiwa na wale ambao watalazimika kujenga tena".

"Katika kile ambacho ni wakati mgumu kwa watu wa Haiti, Nimefadhaishwa na tetemeko hili," alisema.

USGS awali ilionya kuwa tetemeko hilo huenda likasababisha maelfu ya vifo na majeruhi. Pia limesema kuwa mitetemeko mengine sita ilisikika katika maeneo hayo ikiwemo moja lenye ukubwa wa 5.1.

Picha zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha majengo yaliyoporomoka na mkusanyiko wa vifusi baada ya tetemeko hilo.

Leila Bourahla, Mkurugezi wa shirika la Haiti la Save the Children, ameliambia gazeti la New York Times kwamba itachukua siku kadhaa kutathmini uharibifu lakini "ni wazi kuwa hili ni janga kubwa la kibinadamu"


#Bbc Swahili 







0/Post a Comment/Comments