Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ni moja
ya vituo 550 vya chanjo ya UVIKO — 19. Kabla ya chanjo Taasisi kupitia Prof.
Mohamed Janabi na madaktari wengine huwa inatoa elimu ya chanjo na ugonjwa wa
UVIKO – 19.
Kama moja ya kituo cha kutoa chanjo ya UVIKO –
19 Taasisi imekua ikitoa elimu na huduma ya chanjo kwa wananchi wote
wanaotembelea JKCI kwa ajili ya kupata huduma hiyo lakini pia imefanya hivyo
kwa wafanyakazi wa Tanzania International Container Terminal Services – TICTS,
Shule binafsi ya International School of Tanganyika – IST tawi la Upanga na leo
itafanya hivyo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania.
Katika Taasisi chumba cha wagonjwa wanaohitaji
uangalizi maalum kina jumla ya vitanda tisa (9) tu, na mara zote wagonjwa
wanaolazwa katika chumba hicho ni wale waliotoka katika upasuaji wa moyo tu.
Taasisi hailazi mgonjwa mwingine yeyote ICU ambaye hajatoka kwenye
upasuaji. Kwa kipindi cha mwezi sasa ICU haijawahi kuwa na wagonjwa zaidi ya
watano kwa wakati mmoja.
Taasisi bado inahimiza wananchi kujitokeza
kwenye semina za chanjo ya UVIKO — 19 maana semina hizo zinatoa fursa ya
kuuliza maswali na baada ya hapo kwa ridhaa yako utafanya maamuzi ya kuchanja.
Tunashauri wanahabari kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya UVIKO – 19 na kuendelea kuhamasisha watu kuja kuchanjwa
Post a Comment