WANANCHI WATAKIWA KUHESHIMU MAENEO YA HIFADHI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi kuheshimu maeneo ya hifadhi kwa faida ya jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo kwa kuwa ni vyanzo vya maji na kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla.


Amesema hayo leo Agosti 31,2021 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Karatu, Mhe. Daniel Awack aliyehoji kuhusu mpango wa Serikali wa kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Kata ya Mbulumbulu katika kijiji cha Lositete.


Akitoa ufafanuzi kuhusu hoja hiyo, Mhe. Masanja amesema kuwa mgogoro huo ulitatuliwa kwa kushirikisha mamlaka mbalimbali za Serikali zikiwemo Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya ya Karatu, Monduli na Ngorongoro, Wataalam kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Wilaya za Karatu, Monduli na Ngorongoro na Wahifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.


Ameongeza kuwa wananchi wa Kijiji hicho walivamia eneo la hifadhi ya Ngorongoro na Serikali iliwarudisha katika maeneo yao.

0/Post a Comment/Comments