WATANZANIA WATAKIWA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA MAKUMBUSHO NA MALIKALE

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga 

..............................................................

NA MUSSA KHALID

Wadau mbalimbali nchini wametakiwa kujitokeza kutembelea vituo vya makumbusho na Malikale ili wapate elimu ya kuifahamu asili yao ya masuala ya kale na historia na kuboresha utalii wa ndani.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga wakati akizungumza katika kikao cha baraza la wafanyakazi wa makumbusho ya Taifa ambacho kimefanyika Mikindani Mkoani Mtwara kwa lengo la kujadili mpango mkakati wa utekelezaji wa majukumu katika mwaka 2021/2022.

Dkt Lwoga amesema kwa mwaka uliopita wamepata mafanikio kwa kuongezeka kwa wageni laki moja na elfu arobaini na nne (144,000) ikiwa ni ongezeko la mwaka uliomalizika hivyo ni chachu kwa watumishi wa Makumbusho hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuongeza wageni zaid.

‘Hii ni kama chachu kuona taasisi inaweza kujitangaza zaidi hivyo ni wakati wakufanya kazi zaidi ili kuyafikia malengo la Milioni mbili  lakini pia kuongeza mapato kufikia Bill 6 kwa miaka mitano ndani ya Makumbusho ya Taifa’amesema Dkt Lwoga

Aidha Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wadau kuonyesha uzalendo na kujivunia sifa na utaifa wa urithi wa nchi yao kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali sambamba na kushiriki katika matamasha ambayo yamekuwa yakiandaliwa na Makumbusho ya Taifa.

Dkt Gwakisa Kamatula ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Azimio la Arusha amesema kikao hicho kimeongeza hamasa ya utekelezaji wa majukumu ambayo wamejipangia.

Kwa upande wake Afisa Mipango wa Makumbusho ya Taifa Neema Mbise amesema kikao hicho kimeto mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti wa mwaka 2021/2022 lakini kuhamasisha wajumbe kuonyesha uwezo wao katika ufanyaji wa kazi ili kufanikisha malengo waliyojiwekea.

0/Post a Comment/Comments