Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, akitoa maoni
yake katika kuboresha mkakati wa miaka 10 wa ubidhaishaji Kiswahili ndani na je
ya nchi katika kikao cha kuupitia
mkakati huo baina yake na watendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa
(BAKITA) jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, (katikati) akifuatilia maelezo juu ya mkakati wa miaka
10 wa ubidhaishaji Kiswahili ndani na je ya nchi wakati wa kikao cha
kuupitia mkakati huo baina yake na
watendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jijini Dar es Salaam.
Na. Projestus Binamungu GCU- WHUSM
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameliagiza
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kuwashirikisha wadau wa lugha ya
Kiswahili katika kuboresha Mkakati wa Taifa wa Miaka 10 wa ubidhaishaji
Kiswahili na mara baada ya hapo uzinduliwe na kuanza kutekelezwa.
Waziri
Bashungwa ametoa agizo hilo katika kikao na watendaji wa Baraza hilo
kilichofanyika ofisi za BAKITA Jijini Dar es Salam ambapo aliambatana na Naibu
wake Mhe. Pauline Gekul.
Pamoja
na kuagiza ushirikishwa wa wadau katika uboreshaji wa Mkakati huo, Waziri
Bashungwa pia amewaagiza BAKITA kufanya maboresho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuongeza
ufunguzi wa vituo maalum vya kufundishia lugha ya Kiswahili na Utamaduni wa
Mtanzania katika nchi mbalimbali Duniani.
Mkakati
huo unaopendekezwa na BAKITA unalenga kubidhaisha lugha ya Kiswahili ndani na
nje ya nchi kuanzia mwaka 2021-2031 ambapo lugha hiyo kwa miaka ya hivi
karibuni imeanza kutumika maeneo mbalimbali duniani.
Kwa
mujibu wa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bi.
Consolata Mushi, baada ya kupokea maelekezo viongozi hao, hatua inayofuata ni
kuwapitisha wadau wa Kiswahili katika mkakati huo kabla ya kuuwakilisha kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi
kwa ajili ya hatua zaidi za kiutendaji na utekelezaji wa mkakati huo.
MWISHO


Post a Comment