Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge
NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa
ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam limewataka Wenyeviti wa mitaa kutokuwa sehemu
ya migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwenye maeneo yao.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo na Mwenyekiti wa baraza hilo Songoro Mnyonge wakati akizungumza kwenye kikao cha Robo ya nne ya mwaka baada ya kuibuka mjadala wa watu kuondolewa katika maeneo waliohamishwa kufuatia kufanyika kwa operesheni katika Kata ya Mabwepande.
Mstahiki Meya Songoro amesema baadhi ya maeneo mengi yenye changamoto ya migogoro ya ardhi wanaohusika kuwaweka watu kiholela katika viwanja ni Wenyeviti wa serikali za mitaa hivyo amewataka wafate taratibu kwani hawana mamlaka hiyo.
‘Asilimia kubwa ya hawa ambao wamekuwa kwenye maeno hayo sisi waheshimiwa madiwani hatujahusika kwa njia moja ama nyingine kuwaweka kwenye maeneo hayo ailimia kubwa waliohusika ni wnyeviti wetu wa serikali za mitaa na wananchi wamkuwa wakiambiwa wasifany hivyo lakini wanafanya’amesema Meya Songoro
Aidha akizungumzia mgogoro wa Mabwepande,
Mstahiki Meya Songoro amesema serikali itaendelea kuwaondoa watu wasiokuwa na uhalali
ili waweze kufata taratibu na sheria katika maeneo yao.
Wajumbe wa baraza hilo akiwemo Diwani wa Kata
ya Kunduchi Michael Urio wameomba kushirikishwa katika masuala mbalimbali
yanayotendeka katika kata zao ili kukomesha vitendo hivyo vya maeneo kuuzwa
kiholela.
Hata hivyo Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa
na watendaji wa idara mbalimbali kutoka katika Manispaa hiyo kimepitisha na
kuthibitisha Muhtasari wa kikao kilichofanyika Mei 19 mwaka huu.

Post a Comment