ZAIDI YA 140,000 WAMEPATA CHANJO TANZANIA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Dorothy Gwajima amesema hadi kufikia Agosti 10, mwaka huu jumla ya Watanzania 140,000 walikuwa wamepatiwa chanjo ya Ugonjwa wa Corona kwa awali ya kwanza.


Alitoa takwimu hizo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua mdahalo wa kitaifa kuhusu Virusi vya Corona, uliohusisha taasisi za serikali, wataalamu wa afya na waandishi wa habari.


Dkt Gwajima alisema baada ya kupokea chanjo ya Johnson & Johnson, serikali itapokea chanjo zingine nne kwa ajili ya matumizi ambazo ni Pfizer, Moderna, Sinopharms na Sinovac.


Aliongeza kuwa awamu ya pili ya chanjo ya mpango maalumu kwa nchi maskini COVAX, itawasili nchini wakati wote ndani ya mwezi huu.


Cc times fm

0/Post a Comment/Comments