BASHUNGWA AWATAKA WATAYARISHAJI NA WAADAAJI KUTENGENEZA FILAMU ZENYE MAFUNZO


Na Brighiter Masaki

Mtanzania Digital

Serikali kupitia Bodi ya filamu nchini imezindua rasmi Tuzo za Filamu kwa mara ya kwanza zilizopewa jina la Taffa.


Akizungumza na waandishi, wasanii, watayarishaji wa Filamu pamoja na wadau wa Filamu Waziri wa Utamaduni, Sanaa, na Michezo Innocent Bashungwa amesema katika Serikali inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kupitia Maelekezo yake inaleta Tuzo kwa mara ya kwanza kitu ambacho hakikuwahi kuwepo hapo awali.


Bashungwa ameeleza kuwa Tuzo zitakuwa ni endelevu na zitasimamia haki kwa kuwa zitaongeza hamasa katika tasnia ya filamu,na kwa Mwaka huu zitajikita katika kutazama mapungufu ili kwa miaka ijayo ziwe katika ubora mkubwa.

 

Hata hivyo Bashungwa ameeleza kuwa Serikali imefanikiwa kuziweka katika eneo moja Taasisi za Bodi ya filamu, Cosota na Baraza la Sanaa (BASATA) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za Wadau wa Sanaa,ambapo taasisi hizo zipo kivukoni katika Jengo la Utumishi jijini Dar es salaam.


Kwa upande wake Kilonzo Kiagho alifafanua moja ya malengo kuanzisha tuzo hizo ni kutambua mchango wa wanatasnia wa filamu wanaofanya kazi nzuri ili kuongeza chachu katika Sekta ya filamu.


Wasanii watembee kifua mbele wajitokeze kwa wingi kufanya uwasilishaji wa Filamu zao kwani kilele Cha tamati Cha kukusanya ni Septemba 26 mwaka huu na Mchakato huo umeanza rasmi na tupokea katika ofisi za Bodi ya filamu ."


Pia kiagho amefafanua zaidi kuwa tuzo hizo hazina upendeleo zina vipengele ambavyo wasanii wataweza kutuma ushiriki wao na hatimae kufikia kilele Cha Fainali mapema novemba 6 mwaka huu.


Miongoni mwa vipengele hivyo ni Msanii anaechipukia kwa upande wakike na wakiume,Mchekeshaji Bora wa vichekesho wakike na wakiume,Filamu Bora ya mwaka.




Waziri wa Utamaduni, Sana'a na Michezo Innocent Bashungwa akizungumza na Waandishi Wahabari wakati wa ufunguzi wa Tuzo za Filamu kwa mara ya kwanza nchini zilizoandaliwa na Bodi ya filamu ikishirikiana na Serikali


Katibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya filamu nchini akitoa ufafanuzi jinsi gani wasanii wataweza kushiriki katika Tuzo hizo ambazo ni kwa mara ya kwanza zimeandaliwa huku akifafanua zaidi kuwa ni za haki

0/Post a Comment/Comments