.............................................................
NA HERI SHABAN
MKUU wa Wilaya Ilala Ng 'wilabuzu Ludigija
ametatua mgogoro wa ARDHI Kifuru kata ya Kinyerezi Wilayani Ilala kwa kuagiza
Maafisa ARDHI kuhakiki upya eneo hilo na kumaliza changamoto iliyokuwepo zaidi
ya miaka kumi
Akizungumza katika kikao cha wananchi Mtaa wa
Kifuru Kata ya Kinyerezi Wilaya Ilala Arch, Ludigija alisema kuanzia jumatatu Maafisa
ARDHI watahakiki upya eneo na kila mtu atabaki na eneo lake ambalo anamiliki
bila kuwekewa vikwazo.
"Wataalam wa Wilaya na Maafisa ARDHI
watashirikiana kumaliza mgogoro huu mara moja pale katika changamoto ofisi
yangu ipo wazi njooni nitawasaidia kila alhamisi ni siku yenu wananchi ya
kusikiliza kero nipo Ofisini na namba yangu mda wote wa kazi ipo wazi "
alisema Arch, Ludigija
Arch ,Ludigija aliwataka wakazi wa
Kinyerezi wakiuza maeneo ya ardhi wafuate michoro ya ramani na kujiepusha
na mgogoro ya mara kwa mara
Aliwataka wananchi wa Wilaya Ilala wanaponunua
ardhi au Mali yoyote wawashirikishe wake zao kwa ajili ya kuja kuwasaidia
.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ,Tabu Shaibu ,Maafisa
Ardhi,Wanasheria ,Wataalam mbalimbali na wwanasheria
Kwa upande wake Diwani wa Kinyerezi Leah Mgitu
ametoa kilio chake Serikali kuhusiana na msitu wa Nyuki kwa sasa imekuwa
kichaka watu wanatupwa katika pori hilo sio msitu wa nyuki hivyo
ameomba Serikali kulichukua poli hilo walisafishe libadilishwe matumizi
litumike kwa huduma za jamii
Diwani Leah ameomba Serikali kuchukua hatua za
haraka kulipatia ufumbuzi suala la msitu huo wa nyuki ambalo linahatarisha
usalama wa watu na Mali na makazi.
Leah alitaka wananchi wake na Wapiga kura wa
Kinyerezi wasisumbuliwe ajalizishwa na kitendo cha Kufungwa kwa akaunti ya
mradi wa kurasimisha makazi
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salam Tabu Shaibu amemsimamisha Mkandarasi wa Taka Kata
Kinyerezi kwa kukosa sifa ya kazi hiyo akidaiwa kulalamikiwa na wanachi
kutokana na huduma yake anayotoa .
Pia Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Tabu Shaibu alisema Serikali inatarajia kupandisha hadhi zahanati ya Kinyerezi kuwa kituo cha afya changamoto zilizolalamikiwa za zahanati hiyo zinashughulikiwa.


Post a Comment