Vituo 26 vya mafuta ambavyo Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati Tanzania (Ewura) ilitangaza kuvifungia katikati ya Agosti, 2021 kwa kile kilichoelezwa kutoweka vinasaba kwenye mafuta vimefunguliwa.
Ewura ikishirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walisema baadhi ya vituo vya mafuta vinavyomilikiwa na kampuni sita za mafuta vimekiuka maelekezo hayo, hatua ambayo imetafsiriwa kama ukwepaji wa kodi.
Kulingana na sheria, mafuta ambayo hayaweki vinasaba ni yale yanayokwenda nje ya nchi na yanayotumika kwenye miradi mikubwa hivyo hupata msamaha wa kodi.
Titus Kaguo ambaye ni Meneja Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa EWURA, amesema kampuni hizo tayari zimefanyia kazi dosari, na wanaweza kufungua baada ya kulipa faini na ushuru uliodaiwa na TRA.
#TimesFMDigital

Post a Comment