JAJI MUTUNGI:VIKAO HIVI VITASAIDIA KUWEKA SULUHU BAINA YA VYAMA VYA SIASA NA JESHI LA POLISI.

Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi akizungumza leo na waandishi wa habari  jijini Dar es salaam

.....................................................


 NA MUSSA KHALID DA ES SALAAM
 

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatarajia kukutana na wadau mbalimbali wa vyama vya Siasa likiwemo Jeshi la Polisi kwa lengo la kuweka majadiliano ya kuwa na maridhiano kati ya Jeshi hilo pamoja na vyama vya siasa katika ufanyaji wa shughuli zao.

Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Jaji Francis Mutungi ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake ambapo amesema nia ya vikao hivyo ni kuweka mazingira rafiki na maelewano baina ya vyama Siasa.

Amesema pindi alipokutana na wanahabari Tar 6 mwezi Juni kuna baadhi ya watu wamejadili na kutoa hoja zao hivyo alikutana na Jeshi la Polisi,TCD pamoja na Mwenyekiti wa baraza kwa lengo la kushauriana ili zoezi hilo liwe na uzito.

Aidha Jaji Mtungi amesema Septemba 23 mwaka atafanya kikao cha Ofisi ya Msajili na Jeshi la Polisi kwa lengo la kujadili na kupata ufumbuzi juu ya malalamiko yanayotolewa na baadhi ya vyama vya Siasa katika ofisi hiyo.

‘Baada ya kamati ya uongozi kukaa huwa inapanga tarehe ya baraza lenyewe na sio kamati tu ndio inaamua kupanga bali inaongozwa na kanuni ya baraza la vyama siasa ambapo kanuni ya 24 ndio inayoeleza kwamba kamati ya uongozi itapanga natehe ya baraza kwa kutoa notisi siku 14 na kikao hiki kitafanyikia Dar es salaam hivyo tar 13 mwezi wa 10 baraza litakwenda kufanyikia Zanzibar’amesema Jaji Mutungi

Msajili huyo amesema kikao cha wadau kitaendeshwa bila ya kuepo upendeleo kwani utaendeshwa na Waziri ambaye hana mafungano ya vyama siasa ili kutia fursa kwa vyama vya Siasa kuelezea chagamoto zinazowakaba na kufikia Maridhiano.

Ikumbukwe kuwa vikao hivyo  vinakuja ilhali kuwa bado kunamalalamiko ya baadhi ya wadau wa vyama vya Siasa kushidwa kufanya mikutano yao kwa kueleza Jeshi la Polisi kuwaingilia.

0/Post a Comment/Comments