KAMPUNI YA WLC YAJA NA SULUHISHO LA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA

Mkuu wa Kitendo cha Masoko wa Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC)Agnes Daniel (kulia) na Afisa Masoko wa (WLC) Apaisaria Godvice (kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam (picha na Emannuel Mbatilo)

.....................................................................................

NA MUSSA KHALID

Wakati dunia ikihangaika na janga la UVIKO 19,Kampuni ya World Logistics Company Limited (WLC) imekuja na suluhisho la kuwasaidia wajasiriamali na wote wanaoagiza bidhaa zao nje ya nchi kupata bidhaa zao kwa urahisi.

Hayo yamejiri wakati kumekuwepo na changamoto ya uwepo wa Janga la UVIKO 19 hasa kwa wafanyabiashara ambao ambao hawajachanja hali ambayo imepelekea kampuni hiyo kushiriki kwa kurahisisha huduma na kulinda afya za watanzania.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam,Mkuu wa Kitendo cha Masoko kampuni ya (WLC) Agnes Daniel amesema wameanzisha huduma iitwayo Cargo Pickup&Delivery Service ili kurahisisha huduma kwa wafanyabiashara kwa kutafuta mzigo au bidhaa kutoka kiwandani na sehemu zilipoagizwa kwa kuzisafirisha kuja nchini.

‘Katika sekta yetu hii ya lojistiki na usafirishaji,wahanga wakubwa ni wafanyabiashara na wajasiriamali wanaoagiza bishaa zao kutoka nje ya mipaka yetu hivyo tumeona ili ndugu zetu wasiendelee kuumia tumeamua kuja na suluhisho’amesema Agnes

Kwa upande wake Afisa Masoko wa (WLC) Apaisaria Godvice amesema wameanzisha huduma hiyo kwani itamsaidia mfanyabiashara aliyeagiza mzigo kuepuka usumbufu,gharama za safari,hotel na michakato mingine ambayo itamgharimu pesa pamoja na muda

Hata hivyo imeelezwa kutokana na uzoefu wa kampuni hiyo kwa miaka 15 wamekuwa wakiwasaidia wafanyabiashara,wajasiriamali,makampuni na watu binafsi wanaonunua bidhaa nje ya Tanzania.

0/Post a Comment/Comments