Afisa Muendeshaji Mkuu wa Kampuni ya
Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Utalii Kilimanjaro International Tourism
and Safaris (KITS) Francis Malugu (kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya
Taifa ya Utalii (TTB) Felix John (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Wellwork Hotel Sameer Ismail (kushoto)
.............................................................
NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Takriban mawakala wa utalii zaidi ya 30 kutoka nchini Marekani,Lithuania na Ufaransa wanatarajiwa kuja nchini kwa ziara ya mafunzo ya mazao ya utalii pamoja na matembezi.
Imeelezwa kuwa Mawakala hao wataingia nchini kuanzia Novemba 23 mwaka huu
kufuatia kupata taarifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh
Hassan kushiriki kwenye kutengeneza makala ya Filamu ya Utalii Royal Tour ambapo
atakuwa muongozaji mkuu wa zaira hiyo ya kufanya utalii.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati
akitambulisha ujio wa watalii hao,Afisa Muendeshaji Mkuu wa Kampuni ya
Kimataifa inayojihusisha na masuala ya Utalii Kilimanjaro International Tourism
and Safaris (KITS) Francis Malugu amempongeza Rais wa kutangaza Tanzania kwani
itasaidia kuongeza nguvu kuvutia utalii na kukuza uwekezaji.
"Mara baada ya kupata
taarifa mapema za utengenezaji wa makala hiyo ya filamu na kwamba Rais Samia
Suluhu Hassan ndiye atakayekuwa muongozaji mkuu, tuliwataarifu mawakala wa
Utalii katika vyama vya utalii duniani ambavyo KITS ni mwanachama wake na zaidi
ya mawakala 30 waliomba na kuthibitisha kuja kuitembelea Tanzania, Novemba
mwaka huu." Ameesema Malugu.
Aidha amesma matarajio yao kuwa
makala hiyo inayorekodiwa na Mh.Rais Samia itakuwa nyenzo muhimu katika
shughuli za utangazaji zinazoendelea ili kuisaidia nchi kufikia lengo la
watalii millioni 5 na mapato ya dola za kimarekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025
licha ya kuwepo kwa changamoto za Uviko 19 zinayoikabili dunia.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko Bodi ya Taifa ya
Utalii (TTB) Felix John amesema ujio wa mawakala hao wa utalii ni fursa muhimu
kimkakati katika kuhakikisha wanafikia malengo waliyowekewa ya serikali ifikapo
mwaka 2025 nchi iwe na uwezo wa kuvutia watalii wasiopungua Mill 5 na
kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Sameer Ismail ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Wellwork Hotel amesema wametengeneza Hotel zenye hadhi za kwa lengo la
kuwasaidia wageni wanaowasili nchini kupata hifadhi za malazi katika hotel
hizo.
Hata hivyo Kampuni ya KITS ambayo Makao Makuu yake yapo nchini Marekani imesema itasaidia Filamu ya Utalii kuonyeshwa kwa mawakala hao ili kuvutia utalii katika nchi ya Tanzania.
Post a Comment