..........................................................................
NA SALYM BITCHUKA
Imeelezwa
kuwa ukatili dhidi
ya wanawake na
Watoto hapa nchini umeongezeka
suala ambalo linahitaji
ufumbuzi na hii
ni kwa mujibu ripoti
ya Haki za Binadamu ya
mwaka 2020 iliyotolewa na Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu
nchini.
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo
Matukio ya ukatili dhidi
ya Wanawake yaliyotolewa
na vituo vya polisi
nchini yalikuwa ni 26,544
ikilinganishwa na mwaka 2019 ambapo
matukio yalikuwa ni 23,685 hii
ikiwa ni ongezeko la
asilimia 5.7, Pia vitendo vya
ukatili dhidi ya
watoto kwa mujibu wa
taarifa za jeshi
la polisi viliongezeka.
Hayo yameelezwa leo jijini
Dar es Salaam na
mkurugenzi mtendaji
wa Kituo
cha Sheria na
Haki za binadamu ( LHRC) Anna
Henga wakati wa uzinduzi
wa mbio Maalum
za Haki Marathon
ikiwa ni sehemu
ya kuelekekea Maadhimisho
ya siku ya
kimataifa ya Haki
za Binadamu Disemba kumi
mwaka huu.
Kwa upande
wake mratibu wa
Haki Marathon Deus Mtukamazina na Mkurugenzi
wa Ujengaji uwezo
na uwajibikaji LHRC Felister
mauya kwa pamoja wameleelezea
mbio hizo za Haki Marathon zimelenga
kuwajengea uelewa na kuwawezesha Watanzania
kutambua wajibu wao wa
kulinda haki za
Binadamu nchini.
Mbio za haki
Marathon zitafanyika kwa
njia ya mtandao
kuanzia Oktoba 17 mwaka
huu 2021 na
kufikia kilele Desemba 10 2021
ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya
siku ya Kimataifa
ya Haki za Binadamu na zikitarajia kuwa na washiriki
zaidi ya 1,000 huku
kauli mbiu ya
mbio hizo ikiwa
ni ‘’ HAKI NI MAENDELEO ‘’

Post a Comment