Asema agizo hilo ni kwa Wafanyabiashara Mkoa mzima.
Amtaka DC Ilala na Uongozi wa Machinga kuweka utaratibu mzuri kuwapanga Machinga Kariakoo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amepiga marufuku *ufanyaji wa Biashara Kwenye maeneo hifadhi ya barabara* zote za Mkoa huo baada ya utaratibu huo kuwa *chanzo cha uvunjifu wa amani na ongezeko la ajali.*
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo alipotembelea *Soko la Kariakoo* na kujionea Kero ya *Ufanyaji biashara holela Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu*.
Kutokana na hilo *RC Makalla* amewaelekeza *Mkuu wa Wilaya ya Ilala* kufanya kikao na Wafanyabiashara hao Jumatatu ya *September 13* na kuainisha maeneo ya kuwapeleka wote waliovamia *hifadhi ya Barabara.*
Aidha *RC Makalla* amewaelekeza Kuangalia utaratibu mzuri wa *kufunga na kufungua baadhi ya Mitaa Kariakoo kwaajili ya kufanya biashara* Kutokana na *ufinyu wa maeneo* ili Waweze kupata riziki.
Hata hivyo *RC Makalla* amesema kwa tathimini aliyofanya amebaini *Hali ya Ufanyaji biashara holela Dar es salaam ipo kwa kiwango kikubwa na kuwanyima watembea miguu haki zao za msingi.*
Pamoja na hayo *RC Makalla* ameelekeza Manispaa zote za Mkoa huo kuweka *Vibao vya kuzuia biashara Kwenye maeneo ya watembea kwa miguu.*





Post a Comment