Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa karakana kuu ya
Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa katika eneo la Kwala mkoani
Pwani wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa reli hiyo kuanzia
Stesheni Kuu ya Dar es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro, Septemba 12, 2021.
Wa nne kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho na
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya treni maalum ya
wahandisi wa kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR) wakati
alipokagua ujenzi wa reli hiyo kutoka Dar es salaam hadi Kilosa mkoani
Morogoro, Septemba 12, 2021. Katikati ni Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shrika la
Reli Tanzania, Masanja Kadogosa. (Pcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuka kutoka kwenye treni ya
wahandisi wanaojenga Reli ya Kisasa (SGR) wakati alipofika kwenye eneo la Kwala
Mkoani Pwani akiwa katika ziara ya kukagua mendeleo ya ujenzi wa reli hiyo
kutoka Dr es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro, Septemba 12, 2021. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa karakana kuu ya
Reli ya Kisasa (SGR) inayojengwa katika eneo la Kwala mkoani
Pwani wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa reli hiyo kuanzia
Stesheni Kuu ya Dar es salaam hadi Kilosa mkoani Morogoro, Septemba 12, 2021.
Wa nne kulia ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Leonard Chamriho na
kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
...............................................................
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande
cha Dar es Salaam hadi Kilosa, Mkoani Morogoro na kusema kwamba ameridhishwa na
hatua ya ujenzi iliyofikiwa.
“Mheshimiwa
Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kukamilisha ujenzi wa miradi yote
iliyoanzishwa, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao, na
tunawahakikishia mradi huu utakamilika kwa wakati.”
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Septemba 12, 2021) wakati akikagua maendeleo
ya ujenzi ya mradi huo katika kituo cha Kwala kilichopo mkoani Pwani, ambacho
kitatumika kama kituo kikuu cha kufanya matengenezo makubwa ya mabehewa na
injini za treni.
“Maendeleo
ya ujenzi huu yanatia matumaini na kazi inaendelea kwa ufanisi na eneo
lililobaki la Pugu Dar es Salaam tunaamini litakamilika kwa wakati,
nimeridhishwa na vituo vya abiria vilivyokamilika.”
Aidha,
Waziri Mkuu amewasihi wafanyakazi wa mradi huo kufanya kazi kwa ufanisi kwani
lengo la Serikali ni kuufikisha mradi huo katika mikoa ya Mwanza, Kigoma,
Katavi katika bandari ya Karema.
“Njia
zote za reli tunataka ziwe za kisasa, hii pia itawezesha kuinua uchumi wa mtu
mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, nchi yetu ni ya kimkakati kwa sababu nchi zote
za jirani zinategemea reli hii”
Aliongeza
kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na
mizigo kwa kupunguza muda wa safari, kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na
mwanza.
Naye, Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa amesema hadi kufikia mwezi
wa nane mwaka huu ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ulikuwa
umefikia asilimia 93.
Hata
hivyo, Mkurugenzi huyo amesema kuwa ujenzi wa kipande cha pili cha Mradi huo
kinachoanzia Morogoro hadi Makutopola (Singida) ulikuwa umefikia asilimia
70.11.
Amesema SGR ikikamilika itachochea mipango ya Serikali ya awamu ya sita katika kutekeleza sera ya viwanda na kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2025.
Post a Comment