Makumbusho ya Taifa nchini imepokea ugeni wa Uongozi na Wataalam wa Makumbusho ya Taifa nchini Malawi ambao utakuwa nchini kwa siku sita ili kupata uzoefu wa namna ya uendeshaji wa shughuli za kimakumbusho.
Akiwapokea wageni hao katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyeyere Dar es Salaam, Mratibu wa program ya wageni hao wa Makumbusho ya Taifa nchini Bi Frida Kombe amesema ni faraja kubwa kuona nchi za nje zinaiona Tanzania kama Mwalimu wa uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na Mambokale.
Wakiwa nchini, licha ya kujifunza shughuli za uhifadhi pia siku ya Ijumaa tarehe 24 September 2021 watapata nafasi ya kutanzama maonesho ya Museum Art Explosion, kufanya Utalii kuzunguka Dar es Salaam na Bagamoyo Mkoani Pwani

Post a Comment