Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amepiga *marufuku ujengaji holela wa Vibanda vya biashara Mashuleni* Kutokana na utaratibu huo *kuhatarisha usalama wa wanafunzi* baadhi ya watu kutumia mwanya huo *kuwarubuni watoto wa shule.*
Kutokana na hilo *RC Makalla* ameamuru Wakuu wa shule kusimamia *kuondolewa kwa Vibanda vyote vilivyojengwa kwenye maeneo ya shule.*
Aidha *RC Makalla* amesema ni vyema Wanafunzi wakapata mahitaji yao kwenye *duka la shule* au ukafanyika *mchujo watu wachache maalumu wa kutoa huduma ambao wanatambulika na uongozi wa shule* ili ata ikitokea tatizo iwe rahisi kujua chanzo Cha tatizo.
*Hayo yote yamejiri wakati wa Mwendelezo wa ziara ya RC Makalla ya utatuzi wa Migogoro ya Wananchi Jimbo kwa Jimbo ambapo leo ilikuwa zamu ya Wananchi wa Jimbo la Segerea*.



Post a Comment