Watu wawili wamefariki Dunia kwa ajali iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki.
Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo leo Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa Ajali hiyo ilitokea jana tarehe 08,Agoust majira ya saa 21:20 usiku katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea
magari,ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya
Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan(17),Mkazi wa Gerezani,
akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la
mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon
lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya
dereva wa pikipiki na abiria.
Kamanda Muliro amesema kuwa Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa
pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo
walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa
pikipiki kutii sheria za usalama barabarani husasani taa za kuongozea
magari,kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za
Mwendokasi.

Post a Comment