Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (Bara) Mheshimiwa Christina Mndeme.
........................................................
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi (Bara) Mheshimiwa Christina Mndeme amemaliza ziara yake katika wilaya
ya Ruangwa ikiwa sehemu ya Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama hicho pamoja na
Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Lindi.
Ziara hiyo yenye lengo la kukagua na
kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 -2025 imekuwa
na mafanikio makubwa sana.
Akiwa wilayani Ruangwa Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara) alitembelea Mradi wa Maji Nandeje uliotekelezwa kwa mfumo wa
force account na wenye uwezo wa kuhudumia wakazi 1000.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM ametoa
maagizo kwa Wakala Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)
kujenga vituo zaidi vya maji kijijini hapo kwani kituo kimoja hakitoshi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Ruangwa amesema wamepokea maelekezo ya Serikali na kusitokee kusimamishwa kwa
mradi wowote wa Serikali kusimamishwa kwa sababu ya huduma ya maji kutolipiwa.
Mradi huo wa maji ambao awali
Serikali ilitoa fedha shilingi 54,345,762.50 lakini zilizotumika ni shilingi
39,042,905.22 ikiwa sawa na asilimia 71.84% ya fedha zilitotengwa.
Naibu Katibu Mkuu pia alipata nafasi
ya kutembelea ujenzi wa shule ya Sekondari Mandarawe, Vijana 23 wa CCM wenye
mradi mzuri wa kufyatua matofali na kukagua maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa
mpira wa Majaliwa Stadium.
Mwisho Naibu Katibu Mkuu alikutana na kufanya Vikao na Wenyeviti wa Mashina ambapo alihimiza kuongeza wanachama, kufanya vikao na kuwajibu wapinzani wenye nia mbaya kwa hoja za msingi ili kuepusha kuenea kwa upotoshaji.

Post a Comment