Baraza
la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira –NEMC limewataka wamiliki wa vituo
vya mafuta pamoja na wanaohitaji kufanya uwekezaji huo kuzingatia usalama wa
wananchi ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wananchi wa eneo husika ili kuondoa
kero na migogoro isiyofaa pamoja na kuhatarisha maisha yao.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo Dkt Samueli Gwamaka amesema
hatari hizo ni pamoja na vituo hivyo kushika moto ambapo ameongeza kuwa
muwekezaji yoyote atakayekiuka sheria hizo atachukuliwa hatua za kisheria.
Amesema
kumekuwa na ombwe la muingiliano wa
shughuli inayotokana na miradi hiyo huku akitoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano
pale ambapo wanaona mradi unaanzishwa bila kufuata sheria.
Sambamba
na hilo Dkt Gwamaka amewataka wawekezaji wote ambao bado hawajasajili miradi
yao kuanza kusajili miradi yao katika baraza hilo ili kuepuka faini.
Mwenyekiti
serikali ya mtaa wa Goba Mustafa Mponda amekiri uwepo wa changamoto za kupata
ya kupata ushirikiano kutoka kwa wamiliki wa vituo hivyo hasa katika miradi ya
maendeleo kama vile shule.
Kwa
upande wao baadhi wananchi wa mtaa wa
Goba wamesema kuwa licha ya ujenzi wa vituo hivyo lakini swala utoaji wa elimu
juu ya kujikinga na madhara ya ujenzi wa vituo hivyo haitolewi.
Hivi karibuni Baraza la Taifa la uhifadhi na usimamizi wa mazingira –NEMC limezitoza faini ya shilingi bilioni 5.1 kampuni za uuzaji na usambazaji wa mafuta kwa kushindwa kufanya tathmini ya athari kwa mazingira –TAM.

Post a Comment