RAIS DKT MWINYI AFURAHISHWA NA UTAYARI WA INDIA KUIMARISHA SEKTA YA VIPAUMBELE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan
....................................

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefurahishwa  na utayari wa Serikali ya India katika kuendeleza na kuimarisha sekta za vipaumbele vilivyowekwa na Serikali ya Awamu ya Nane hasa katika Uchumi wa Buluu.
 
Rais Dk. Mwinyi alieleza hayo leo Ikulu Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Mhe. Binaya Srikanta Pradhan, aliyefika Ikulu kujitambulisha kwa Rais.
 
Katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Pradhan kwamba Serikali ya India ina uwezo mkubwa wa kuvitumia vipaumbele vilivyopo hasa katika kuitumia fusra ya Uchumi wa Buluu kupitia sekta ya utalii, usafirishaji, uvuvi, bandari, mafuta na gesi asilia.
 
Hivyo, Rais Dk. Mwinyi alimueleza Balozi Pradhan kuwa sekta hizo zote zilizopewa msukumo katika uchumi wa Buluu zinahitaji uwekezaji kutoka Serikali ya India hatua ambayo pia, itapanua soko la ajira hasa ikizingatiwa kwamba  kwa upande wa sekta ya uvuvi kunahitajika viwanda vya kuchakata samaki ambavyo vitatoa ajira. 
 
 

 

0/Post a Comment/Comments