RAPCHA AMEACHIA RASMI ALBAMU YA MWANANGU 99 BOOMPLAY


Na Brighiter Masaki

Mtanzania Digital 


Msanii wa Hip Hop wa Cosmas Paul 'Rapcha' aachia albam yake ya kwanza aliyoipa jina la 'Wanangu 99'.


Akizungumza na Mtanzania Digital jijini Dar es salaam, Mara baada ya kuiachia albam hiyo Rapcha ameeleza kwa namna Mashabiki walivoupokea wimbo wa Lisa na kwa kipindi cha Miezi mitatu tu  na kufanya vizuri na kushika chati za juu za Muziki wa Bongofleva .


"Kwa mara ya kwanza wimbo wangu wa "Lisa"  umeweza kufikisha watazamaji milioni 1.5 kwenye mtandao wa YouTube.


Aidha,Rapcha amempongeza Mtayarishaji wa ngoma kutoka Bongo records ,P funky na kuchukua jukumu la kutayarisha na kusimamia albam hiyo na nyimbo zote zimefanyika chini ya bongo records.


Hata hivyo Rapcha amefafanua ujio wa Muendelezo wa wimbo wake wa Lisa two na kuwataka Mashabiki kusubiri ujio huo wa kisa chenye ukweli na chenye Mafunzo ndani yake.


Albam ya Wanangu 99 inabeba jumla ya nyimbo 10 ikiwemo Majani,Go Rapcha,unajua vibex remix,Nitakucheki,Kama unae,Tunajimwaga na zingine nyingi akiwashirikisha wasanii wanne akiwemo Femi one,King Kaka,Mapanch na Kid Golden. 


Kwa upande wake Meneja uhusiano wa Kampuni ya Boomplay Harrison Lwanga Kazi yetu kubwa ni kutoa Ushirikiano wa wimbo za wasanii mbalimbali.


"Tutahakikisha tunatoa nafasi kwa Mashabiki zake kusikiliza albam hiyo kupitia Boomplay na itadumu kwa wiki 2.

0/Post a Comment/Comments