RC MAKALLA AISHUKURU LIONS CLUB KWA MSAADA WA MADAWATI NA MAJI





- Atoa *Miezi mitatu kwa wavamizi wa Shule ya msingi Mzinga B kuondoka.*


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amepokea msaada wa *Madawati 200* kutoka *Club ya Lions* ya Jijini humo kwaajili ya Wanafunzi wa *shule ya Msingi Mzinga B* iliyopo Halmashauri ya Jiji la Ilala ambapo *ametoa siku 90* kwa wavamizi wa Shule hiyo kuondoka.


*RC Makalla* ametoa agizo hilo Mara baada ya *kupokea Malalamiko* kutoka kwa *Wanafunzi na Walimu* wa shule hiyo Waliolalamikia *Ufinyu wa eneo* la Shule baada ya zaidi ya *Wavamizi 24* kujenga nyumba ndani ya eneo hilo na kusababisha *Kukosekana kwa Maeneo ya Kuendeleza Majengo na eneo la michezo* ambapo tayari *Serikali imeshinda kesi* lakini mpaka Sasa *wavamizi bado hawajaondoka.*


Kutokana na hilo *RC Makalla* ametoa maamuzi ya *busara* ya kuwataka Wavamizi hao *kuondoka ndani ya siku 90 kuanzia Sasa* ili kupisha eneo hilo litumike kwaajili ya *Ujenzi wa Vyumba vya madarasa na maeneo ya michezo.*


Aidha *RC Makalla* ametoa maelekezo kwa *Halmashauri zote* za Mkoa huo kufanya *Maoteo* ya idadi ya Wanafunzi *wanaohitimu na watakaoandikishwa* kujiunga darasa la kwanza na kuanza Ujenzi wa madarasa ili kuepuka *suala la uhaba wa madarasa*.


Hata hivyo *RC Makalla* amepokea changamoto ya *mahitaji ya Vyumba vinne vya madarasa* Katika shule hiyo na kuwahakikishia kuwa tayari *Halmashauri ya Jiji la Ilala Imetenga fedha kwaajili ya Ujenzi wa Majengo hayo.*


Pamoja na hayo *RC Makalla* ameipongeza *Lions club* ya Jiji Hilo kwa kutoa mchango huo wa *Madawati, meza za walimu, makabati na kuchimba kisima Cha maji* shuleni hapo ambapo amewaomba Wadau wengine *kuiga mfano huo.*

0/Post a Comment/Comments