RC MAKALLA AJITWISHA MGOGORO KATI YA WANANCHI NA MSITU WA PUGU KAZIMZUMBWI



- Asema *azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kutatua Migogoro ya Wananchi.*


- Ataka *Mgogoro huo kufika Mwisho.*


- Awapa *pole Wananchi kwa Mgogoro wao kudumu muda mrefu.*


- Awataka *TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu.*


- Sasa kukutana na *Wizara tatu za TAMISEMI, Mliasili na utalii na Wizara ya Ardhi kupata ufumbuzi.*


Kufuatia *Mgogoro wa Ardhi wa muda mrefu* baina ya Wananchi na Wakala wa Huduma za Misitu *TFS* juu ya *Msitu wa Pugu Kazimzumbwi,* Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* ameahidi kushughulikia Mgogoro huo *kwa kushirikiana na Wizara tatu zinazohusika.*


*RC Makalla* ametoa ahadi hiyo wakati wa *Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza Migogoro ya Wananchi* ambapo Leo ni zamu ya *Jimbo la Ukonga* ambapo amesema *azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kushughulikia Mgogoro ya Wananchi.*


Miongoni mwa kilio Cha wananchi hao ni *Matukio ya kupigwa, kuteswa na kukamatwa* kwa Wakazi wanaozungukwa na Msitu huo ambapo *RC Makalla* amewaelekeza *TFS kuacha matumizi Makubwa ya Nguvu* na badala yake *busara itumike.*


Aidha *RC Makalla* amesema wakati anaendelea kushughulikia Mgogoro huo ni vyema *TFS ikashirikiana na Wananchi* hao na kupiga marufuku vitendo vya *kukamata Wananchi wa Dar es salaam* na kupeleka *Wilaya ya Kisarawe.*

0/Post a Comment/Comments