RC MAKALLA AWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI MAZINGIRA BORA YA BIASHARA


- Akemea *Rushwa na Urasimu.*


- Asema Serikali ya Mkoa inaunda *One stop Center ya Biashara*.


- Azielekeza *Mamlaka za udhibiti* kuweka utaratibu wa *kuwatembelea wenye Viwanda kwa pamoja kuepuka usumbufu.*


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amewahakikishia *Wafanyabiashara na wawekezaji* mkoani humo kuwa Serikali itaendelea kuweka *mazingira Bora na wezeshi* ya biashara kuenda sambamba na *azma* ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya *Rais Samia Suluhu Hassan* ya kuondoa kero za kibiashara.


Akizungumza wakati wa mkutano wa *shirikisho la Wenye Viwanda* CTI, *RC Makalla* amesema Serikali ya Mkoa ipo hatua ya mwisho ya kuanzisha *One stop Center ya biashara* itakayojumuisha Mamlaka zote za udhibiti ikiwemo *TBS, NEMC, OSHA, TRA, BRELA, Jeshi la zimamoto, Uhamihaji*  ili kupunguza *Urasimu*.


Aidha *RC Makalla* ameelekeza *Mamlaka zote za udhibiti* ikiwemo TBS, NEMC, OSHA, Jeshi la zimamoto, Uhamihaji na nyinginezo kuweka utaratibu wa *kutembelea viwanda kwa pamoja* ili kuepuka *kukinzana* kwa matamko ,maelekezo pamoja *usumbufu wa kupokea wageni kila siku.*


Pamoja na hayo *RC Makalla* ameelekeza *TANROAD na TARURA* kurekebisha *miundombinu ya Barabara kwenye Maeneo ya Viwanda* ili kuondoa kero na changamoto ya *uharibifu wa Magari.*





0/Post a Comment/Comments