RC MAKALLA KUSIMAMIA MABORESHO MNADA WA PUGU






Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* amefanya Mazungumzo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi *Mhe. Mashimba Ndaki* kuhusu Hali ya *Ubovu na uchakavu wa Mnada wa Pugu* na jitiada za *kuboresha Machinjio hiyo* kuwa ya kisasa kuendana na *hadhi ya Jiji la Dar es salaam.*


Mazungumzo hayo yamekuwa na *mafanikio makubwa* baada ya *Waziri Ndaki* kumkabidhi *RC Makalla* jukumu la *kumsimamia na kumbana Mkandarasi* amalize kazi ya kuboresha Mnada huo Kufuatia *Mkuu wa Mkoa kutoridhishwa na Hali ya Mnada huo* wakati alipofanya *ziara* mnadani humo hivi karibuni na kujionea *Kero lukuki.*


Kutokana na hilo Sasa *RC Makalla ameahidi kumsimamia ipasavyo mkandarasi kukamilisha maboresho ya Mnada kwa wakati* ili kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili *wafugaji na Wafanyabiashara Katika Mnada huo.*


Aidha *RC Makalla* amesema Kama Mnada huo utakuwa Katika Hali nzuri itasaidia pia *Machinjio ya kisasa Vingunguti* kupokea mifugo yenye *ubora* na kusaidia upatikanaji wa *Nyama Bora.*


Hayo yote yamejiri wakati wa *mkutano wa Wadau wa sekta ya Mifugo* uliofanyika leo Jijini Dar es salaam ambapo *Mgeni rasmi* alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania *Mhe. Kassim Majaliwa.*

0/Post a Comment/Comments