UNAJUA??
Edouard Mendy!
Wakati akiwa na umri wa miaka 22 aliwahi kuamua kuachana na mchezo wa soka mara baada ya kuona mambo hayaendi.
Hii ilikuwa mwaka 2014 mara baada ya kuachwa na timu ya As Cherbourg ya nchini Ufaransa.
Baada ya kuachwa na timu hiyo, Mendy alijikuta akikaa mwaka mzima bila kusajiliwa na timu yoyote, huku aliyekuwa agent wake akimtelekeza pia kwa kumtumia ujumbe wa kumtakia maisha mema kwa simu tu.
Hali hii ilimfanya aamue kuachana na soka. Kwa mwaka mzima akalipa kisogo soka na kugeukia harakati za kutafuta shughuli nyingine za kufanya, lakini baadaye msukumo na sapoti kutoka kwenye familia yake ilimpa nguvu ya kurejea tena uwanjani na kwenda kuitumikia timu yake ya mwanzo kabisa ya Le havre kwa mwaka mzima bila malipo yoyote.
Kuelekea mwaka 2015 alipata nafasi ya kushiriki majaribio katika klabu ya Marseille na kufanikiwa kupata nafasi kama golikipa wa ziada, akiwa ni chaguo la nne, hapa safari yake ikawa imeanza tena!
Ilipofika msimu wa mwaka 2017/18 akaamua akajiunga na timu ya Reims iliyokuwa daraja la pili nchini Ufaransa ili apate nafasi ya kucheza. Huko akaonyesha uwezo mkubwa huku akiisaidia timu hiyo kupanda daraja, kiasi cha kupachikwa jina la bawabu "The doorkeeper"
Uwezo wake ukaivutia klabu ya Rennes ambayo iliamua kumsajili mwaka 2019, hadi Petr Cech alipomuona na kumpendekeza kwa aliyekuwa kocha wa Chelsea (Frank Lampard). Septemba 24, mwaka 2020 akanyakuliwa rasmi kutua darajani!
Na sasa unapozungumzia kati ya Walinda milango bora kabisa ulimwenguni, ni dhahiri huwezi kuacha kulitaja jina lake. Usiku wa jana amecheza mchezo wa 50 akiwa na klabu ya Chelsea, hajaruhusu bao, na zaidi alikabidhiwa tuzo yake ya mlinda mlango bora wa Uefa msimu wa mwaka 2020/21, yuko mawinguni! Yuko juu!
NB: Pasi na kujali unayopitia! USIKATE TAMAA, PAMBANA...






Post a Comment