SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA VITUO MBALIMBALI VYA AFYA.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za mikoa Na Serikali za Mitaa TAMISEMI Kitengo cha Afya  Dkt.Grace Magembe

.....................................................................

NA MUSSA KHALID

Serikali imesema inaendelea kuboresha vituo mbalimbali vya Afya nchini pamoja na Shule ili kusaidia watanzania kupata huduma kwa ukaribu.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za mikoa Na Serikali za Mitaa TAMISEMI Kitengo cha Afya  Dkt.Grace Magembe katika hafla ya Ufungaji rasmi wa Mkutano wa Kitaifa wa mradi wa USAID Kizazi Kipya.

Dkt Magembe amesema tayari Rais Samia ametenga Bill 37.5 ambazo zimepelekwa kwenye tarafa takriban 220 kwa ajili ya kujenga vituo vya Afya huku msukumo ukiwekwa kwenye mradi unaofuata watu kujiunga katika mifuko ya bima ya Afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la PACT Tanzania Mariana Balampama amesema wataendelea kushirikiana na serikali kuangalia Afua mbalimbali kwani katika miaka 5 wamefanya kazi katika Halmashauri zaidi ya 150 Tanzania Bara pamoja na Zanzibar.

Ananthy Thambinayagam ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Afya kutoka Shirika la USAID nchini Tanzania amesema lengo la mradi huo wa Kizazi Kipya ni kuwasaidia vijana kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya Virusi vya Ukimwi.

Hata hivyo imeelezwa kuwa kupitia mradi huo wa Kizazi Kipya vijana zaidi ya 9000 wameweza kupatiwa ufadhili wa kusoma mafunzo ya ufundi stadi na kupatiwa vifaa vya kuanzisha biashara sambamba na kuungwanishwa na vikundi vya kuweka na kukopa ili kuongeza biashara zao.

0/Post a Comment/Comments