Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Mhe. Geoffrey Mwambe ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imejipambanua kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya Uwekezaji ambapo kwa sasa tayari imefanikiwa katika Uwekezaji wa Maeneo Maalum ya Viwanda.
Ameyabainisha hayo katika Mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Septemba 23, 2021 alipokuwa akitoa taarifa kuhusu juhudi zinazofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu- Uwekezaji pamoja na Taasisi zake katika kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji.
Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Taasisi zake imeendelea kuboresha na kuwezesha uwekezaji nchini kwa kipindi cha mwezi April hadi Septemba, 2021 kupitia Taasisi zilizopo chini yake ambazo ni Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Mhe. Mwambe amefafanua kuwa Ofisi hiyo imeendelea kutekeleza malengo makuu ya uwekezaji ambayo ni Matumizi ya uwezo wa nchi yetu katika kuvutia uwekezaji, Kuhamasisha uzalishaji unaolenga kuchochea mauzo nje ya nchi, Uhamasishaji wa uwekezaji kutoka nje, Kuhamasisha na kuwezesha maendeleo ya teknolojia mpya kupitia uwekezaji, Kuimarisha uwazi katika mfumo wa kisheria na ulinzi wa mitaji ya uwekezaji; na Kuimarisha mfumo wa kutoa vibali vya uwekezaji.
Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara kama Kufungua akaunti za wafanyabiashara nchini zilizokuwa zimefungwa, Hatua ambayo imewezesha kuchochea uchumi na kurudisha imani kwa wafanyabiashara na wawekezaji kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi.
Mhe. Mwambe ametoa wito kwa watumishi wa Wizara za Kisekta kutekeleza majuku,u yao kwa ufanisi na uzalendo ili suala la Uwekezaji amablo ni mtambuka. Hivyo, itaendelea kuimarisha liweze kuchochea maendeleo ya uchumi nchini.




Post a Comment