Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Adam Malima (picha na mtandao)
Baadhi
ya majengo ya Sekondari ambayo yamejengwa kwa umoja wa wanakijiji cha Nkelei
..........................................
NA
MUSSA KHALID
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Nkelei
kilichopo Kata ya Rangwi Wilaya ya Lushoto kwa kujitolea kuiunga mkono serikali
kwa Kujenga Vyumba vya Mdarasa ya Sekondari pamoja na Zahanani ya Kijiji hicho.
Akifanya
Mahojiano na mwandishi wa habari hizi Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwa kuonyesha
ushirikiano kwa wananchi hao amewasisitiza Wakurugenzi katika kupelekea pesa za
ndani za maendeleo watoe kipaumbele kwa maeneo ambayo wananchi wamejitolea
nguvu zao kwa kujenga miradi ya kimaendeleo.
RC
Malima amesema popote wanapohitaji nguvu ya kuwasaidia lazima serikali ya Mkoa
iwaunge mkono ili kufanikisha kwa wakati miradi hiyo ya wananchi ili kuweza
kurahisisha huduma na waondokane na changamoto ya kwenda umbali mrefu kutafuta huduma.
‘Kwanza
wananchi wanaojikusanya wakajenga Sekondari pamoja na Zanahani wanajielewa sana
na ndio maana hata mimi katika kuwepo Tanga huwa nawaambia tukitaka kufanya
maendeleo kwa wananchi tujikite kuwaangalia wananchi ambao wameonyesha jitihada
za maendeleo kwani hata usimamizi watafanya vizuri’amesema RC MALIMA
Aidha
Mkuu wa Mkoa Malima amewaomba wananchi kuendelea kutambua na kusimamia vyema
miradi hiyo ya kimaendeleo ili kuepukana na watu wasiopenda maendeleo kwa
kuingiza tamaa katika miradi hiyo.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Rangwi Ramadhani Issa Lyimo amesema malengo yao
Sekondari hiyo ambayo imejengwa kwan nguvu za wanakijiji ni kuanza kutumia
kuanzia mwezi Januari 2022.
Amesema
katika Mradi huo Halmashauri waliwasaidia mabati kwa ajili ya kuezeka lakini
pia Ushirikiano Mkubwa unatolewa na vijana wa mjini ambao ni wazaliwa wa kijiji
hicho ambao wamehakikisha kila hatua inafanikiwa.
‘Kukamilika
kwa miradi hii kutasaidia kwa wanafunzi ambao wanakwenda sekondari ya jirani
kijiji cha Goka kutawaondolea kutembea umbali mrefu kwenda shule na hivyo
kusoma karibu’amesema Diwani Ramadhani
Ikumbukwe Mwenyekiti wa Maendeleo ya
Kijiji kutoka katika umoja wa kikundi Cha Nkelei na Mabadiliko ambacho Makao
Makuu yake yapo Jijini Dar es salaam Rasuli Chanoga alisema wamepatiwa mabati
hayo 132 ambayo yamesaidia kuezeka madarasa mawili ya awali.
Chanoga alisema kwa mchango huo ambao
serikali iliwapatia ni msaada mkubwa kwao kwani adhma yao ni kuwasaidia watoto
wapate elimu bora lakini pia kuwaondolea adha na changamoto ya kwenda umbali
mrefu kuitafuta elimu.
Aidha Chanoga alisema baada ya kupatiwa mabati hayo matarajio yao mpaka kufika mwezi Januari mwakani madarasa hayo yawe yamekamilika na hivyo wanafunzi kuanza kuyatumia kwa kujifunzia.



Post a Comment