Naibu Waziri wa kilimo husen Bashe ( Mbunge) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kikao
Na Richard Mrusha
Serikali nchini imepiga marufuku matumizi ya kamba za plastiki na magunia kwa taasisi zote za Serikali na kuagiza kutumika kwa kamba zinazotokanazo na zao la Mkonge ili kuongeza soko la uhakika kwa wakulima wa Mkonge.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Hussein Bashe kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Mkutano wa pili wa wadau wa sekta ya Mkonge uliofanyika Septemba 13 mwaka huu Ilonga Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro
Mhe Bashe amesema sio tu matumizi ya kamba za Plastiki zinachangia kwa asilimia kubwa kupunguza soko la Mkonge lakini pia mifuko hiyo inauzwa pasina kuwa na nembo ya ubora na zinazalishwa na viwanda bubu ambavyo havijasajiriwa na Serikali.
‘’…Naiagiza Wizara ya Kilimo kutoa tamko la kisera kuzuia matumizi ya kamba za plastiki katika kufungashia mazao mbalimbali na taasisi zote za Serikali ni marufuku kutumia kamba za plastiki badala yake watumie kamba za katani amesema Bashe.
Aidha Bashe amemwagiza Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa mbegu za Kilimo Tanzania (TARI ) na Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge Tanzania kuhakikisha wanakuwa na Ofisi ndogo ya zao la Mkonge Wilayani Kilosa na waanzishe kitalu cha uzalishaji wa miche ya zao la mkonge kwa ajili ya wakulima wa zao hilo waliopo Mkoani Morogoro.
Katika hatua nyingine Bashe ameitaka taasisi ya utafiti wa mbegu za kilimo Tanzania ( TARI ) kuwasaidia wakulima wadogo kutumia mbinu bora za kilimo ikiwa ni pamoja na kutoa Elimu kwa wakulima ili kuweza kumudu utunzaji wa mashamba na kuwapatia mafunzo ya ugani ya kutumia eneo dogo la shamba litakalotoa mavuno mengi.
Na kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amesema Mkoa wa Morogoro umejipanga vizuri kuwasaidia wakulima wa zao la Mkonge kwa kuhakikisha wanafanya block farming, kuainisha mashamba ya Mkonge na kushirikiana na taasisi ya utafiti wa mbegu za kilimo Tanzania ( TARI ) katika kuwasaidia wakulima kuwapa mashine za kusindika zao hilo la Mkonge.
Sambamba na hayo amewataka wadau na taasisi za fedha Mkoani humo ikiwemo NSSF kujipanga kuleta mashine za kusindika Mkonge ili wakulima wasitumie mashine ndogo zilizopo sasa ambazo haziwezi kutoa Mkonge wenye ubora
Aidha Shigela amewatoa hofu wakulima wa zao hilo kuwa watahakikisha wanawadhibiti wafugaji wanaolishia mifugo mazao yaliyopo kwenye mashamba yao na kuwaahidi kutatua changamoto za wanamya pori aia ya Tembo wanaovamia mazao ya wakulima
Amesema changamoto mbalimbali anazokumbana nazo katika zao la Mkonge akiwemo Mwenyekiti wa wadau wa zao la Mkonge Damian Luhinda amesema changamoto anazokumbana nazo ni ukosefu wa mitaji, ushindani wa bidhaa za Plastiki na kuongezeka kwa kodi.
Na kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Mkonge Bi Mariam Nkumbi ameiomba Serikali kudhibiti changamoto ya Tembo wanaovamia mashamba ya wakulima na kusababisha hasara jambo linalopelekea wakulima hao kukata tamaa ya kuendelea kulima zao hilo.
Mkutanao wa kwanza wa wa Wadau wa uhamasishaji wa zao hilo la Mkonge ulifanyika mjini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa mkutano uliofanyika hapa Kilosa ni mkutano wa pili ambapo Waziri Mkuu amewakilishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.
MWISHO.

Post a Comment