Wanafunzi 26 kutoka shule za Sekondari ya Nyegina, Mugango na Chief Wanzagi wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo kompyuta
.............................................................
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kushirikiana na Tanzania Development Service (TDS) ya nchini Marekani wametoa mafunzo ya kompyuta kwa shule tatu za Sekondari mkoani Mara.
Mafunzo haya yanayoenda sambamba na ufungaji wa kompyuta 30 yanatolewa na Wataalamu pamoja na wanafunzi kutoka DIT, hii ni muendelezo katika kutekeleza dhana ya Mafunzo Vitendo (Teaching Factory) inayotekelezwa katika DIT ambapo wanafunzi wanapata mafunzo kwa vitendo zaidi ya yale ya darasani.
Wanafunzi 26 kutoka shule za Sekondari ya Nyegina, Mugango na Chief Wanzagi wameshiriki kwenye mafunzo hayo yatakayotolewa kwa siku tano.
Matarajio ya DIT na TDS ni kuwa, baada ya mafunzo haya wanafunzi wataweza kupeleka utaalamu huo kwa wengine ambao hawakupata fursa ya kushiriki mafunzo haya.
Mafunzo haya pamoja na kompyuta 30 vimefadhiliwa na Taasisi ya TDS.


Post a Comment