SIMBA SC KUTAMBULISHA JEZI MPYA JUMAMOSI



Na Richard Mrusha

 Klabu ya Simba yatangaza tarehe ya uzinduzi wa jezi mpya kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara mwaka 2021/2022  rasmi Setemba 4 mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.


Akizungumza leo na waandishi wa habari Kaimu Msemaji wa Klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema Simba iliingia mkataba mkubwa na Fred Vunja Bei kwa ajili ya jezi za Simba na waliingia mkataba wa Sh,bilioni mbili.


"Kabla ya Klabu ya Simba kuingia mkataba na Vunja Bei tulikuwa na Umbro na tulikuwa na mafanikio makubwa na Simba ni sehemu ya mafanikio tunafahamu biashara ya jezi na vifaa vya michezo ndio biashara kubwa duniani zaidi ya trilioni 84 zinapatikana katika biashara ya vifaa vya michezo na jezi,"amesema Kamwaga.


Ameongeza kuwa Simba katika kuamini vijana wa Tanzania imeamua kuingia mkataba na Fred Vunja Bei kwa ajili ya jezi na vifaa vya michezo vya Simba, ana maduka kila mahali na yote yatakuwa na jezi za Simba.


Aidha Kamwaga ameweka wazi kuwa Septemba utakuwa mwezi wa Simba kutokana na matukio mbalimbali yatakayoendelea kuanzia leo kuelekea Septemba 19 mwaka huu ambayo itakuwa Simba Day.


Kwa upande wake Fred Vunja Bei amesema kwamba wamepata nafasi ya kuaminiwa na Klabu ya Simba kutengeneza na kuuzaa jezi,hivyo nao wataonesha uaminifu na kuaminika kwao kwa vitendo.


" Simba imetuamini na sisi tutaonesha uaminifu, hakuna jezi ambayo imetengezwa ikavuja hadi sasa,Kwenye mitandao zimewekwa jezi nyingi lakini ukweli jezi yetu haijavuja mpaka sasa jezi zetu za msimu huu zitazinduliwa Septemba 4 mwaka huu.


"Tutakuwa na wadau wa michezo kutoka sehemu mbalinbali, tumejipanga,tunajua ukubwa wa Simba,  hivyo uzinduzi wetu tutaufanya kwa ukubwa wa Simba,kutakuwa na uzinduzi wa aina mbili, Septemba 4 watazindua kuanzia saa 11 hadi saa tatu usiku,na itakuwa live Azam TV, na uzinduzi wa aina ya pili utakuwa wa mtandaoni kwa ajili ya kuuza jezi mtandaoni,"amesema Fred Vunja Bei.


Aidha amesema kuwa upatikanaji wa jezi za Simba baada ya kuzinduliwa utakuwa tofauti na wengine, pale watakapokuwa wametambulisha tu jezi yao basi kokote mwana Simba aliko ataweza kununua jezi muda huo huo wa kuanzia saa moja ya Septemba 4 mwaka huuu kokote aliko.


"Maduka ya Vunja Bei yatakuwa wazi saa 24 na mzigo utakuwa mwingi,hakuna atayakayekosa jezi ya simba na anataka kuuona ukubwa wa Simba kwa kununua jezi,"amesisitiza Vunja Bei.


Ameongeza kwa wale ambao watakwenda Simba Day watakuwa na punguzo la bei ya jezi ,hivyo tiketi za Simba zitauzwa  katika maduka ya Vunja bei.


Na kwa upande wake



MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva Whozu ametunga wimbo maalum kwa ajili ya wanachama,mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Simba ambao unakwenda kwa jina la Simba ni Noma.


Akizungumza leo Septemba 1,2021 Wohzu amesema ameamua kutunga wimbo huo kutokana na mapenzi yake makubwa na klabu ya Simba,yeye ni Simba kindakindaki,hivyo ameamua kutunga wimbo huo.


"Tunafahamiana wengi,mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya,nimekuwa nikitumia talanta yangu katika sanaa ya muziki, hivyo nimeamua kitengeneza wimbo maaalum kwa ajili ya Simba,mashabiki wa Simba ,nimefanya hivyo kwasababu ya wachezaji wa Simba.


"Simba ni bingwa hata wasemeje, nimetumia ubunifu kidogo,sijaimba kwa Singeli bali nimechanganya ladha, nimetumia Singeli kidogo, bongo fleva kidogo na bolingo kidogo, nimechanganya ili kupata kitu kizuri, siko mwenyewe nimemshirikisha Donat Mwanza anayetokea Congo.


"Mwanamuziki huyo ameshawahi kuhiti na Bana Congo, ana wimbo wake ambao umekuwa maarufu sana. Lakini katika mazungumzo yangu na Donat Mwanza ni shabiki mkubwa wa Simba, hivyo haikuwa ngumu kumshawishi, kumshirikisha wimbo huo na tumeufanya kwa Kiswahili,Wimbo unaitwa Simba ni Noma. 


"Simba ni  Noma, wimbo umerekodiwa na upo tayari wimbo ni mzuri sana na umeshatoka, wimbo huo ni maalum kwa ajili ya Simba, ni wimbo wa kushabikia Klabu, kokote uliko mwana Simba tembea kifua mbele,jidai wewe ni mshindi, kikubwa naipenda Simba ,ni Simba kindaki ndaki, tutauwimbo na mashabiki zetu, tutauumba kiubibgwa,amesema Wohzu.


Mwisho

0/Post a Comment/Comments