Mwandaaji
wa tamasha la kumshukuru Mungu na kuliombea Taifa Alex Msama wakati akizungumza
na wanahabari jijini Dar es salaam
..............................................................................
NA
MUSSA KHALID DAR ES SALAAM
Wakazi
wa Mkoa wa Dar es salaam wametakiwa kujitokeza katika tamasha la kumshukuru
Mungu,kuliombea Taifa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan ili taifa liendelee kuwa na amani na maendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mwandaaji wa tamasha hilo Alex Msama
wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema litakwenda sambamba na Kauli mbiu
isemayo ‘Tanzania ni nchi yetu tuipende na tulilinde’.
Msama
amesema Tamasha hilo litafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Octoba 31 mwaka huu likiwa na lengo la kuliombea Taifa la Tanzania hivyo
amewataka wananchi kuendelea kuipenda nchi yao .
‘Nataka
niwaambie wakazi wote wote wa Dar es salaam na MajiranI zake wakiwame wakazi wa
Mkoa wa Pwani wajiandae kushiriki katika tamasha hilo kubwa la kumuombea Rais
Samia pamoja na viongozi wote kwa litakuwa
la historia kubwa nchini kutokana na watanzania’amesema Msama
Msama
amesema wasanii wa Muziki wa Injili wameendelea kufanya mazoezi tayari kwa
ajili ya kushiriki katika tamasha la kumshukuru Mungu ili kutoa hamasa kwa
wananchi wote kuliombea taifa lao.
‘Nataka
niwaambie wote ambao wamejiandaa kuja waje kwa sababu litakuwa ni kubwa sana na
niwaambie waimbaji wa muziki wa injili ambao wamethibitisha kushiriki ni pamoja
na Martha Mwaipaja,Mwimbaji Mkonge Martha Baraka pamoja na Mwimbaji wa
Kimataifa Rose Muhando’ameendelea kusema Msama
Hata hivyo amesema tamasha hilo hailtaishia Dar es salaam pekee bali litakuwa na muendelezo katika Mikoa mbalimbali nane mpaka kumi hapa nchini.
Tamasha la Shukrani limepangwa kufanyika live huku wasanii mbali mbali wa muziki wa injili wakidhibitisha kushiriki tamasha hilo lililopangwa kufanyika Oktoba 31.
Wasanii waliodhibitisha Leo kutumbuiza kwenye tamasha hilo la kuombea taifa, na kumuombea Rais Samia Suluhu ni Martha Mwaipaja, Rose Muhando, na Martha BarakaK
Aidha wasanii hao wataungana na wenzao Upendo Nkone, Boniface Mwaitege, Jessica Honore, Messi Chengula pamoja na Enock Jonas kwenye kambi maalum ya mazoezi ambapo siku hiyo ya tamasha hakuna msanii atakaetumia CD au Flash na badala yake watatumia vyombo live.

Post a Comment