TANZANIA KUWA MWENYEJI ONESHO LA UTALII JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

 




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akitoa rai kwa watanzania hususan wakazi wa Arusha kuhamasika na Onesho la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki mapema leo Jijini Dodoma. Wakwanza Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga na Wapili kutoka ni Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT), Dkt, Abdulla Juma.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na fursa ambazo watanzania watapata katika Onesho la Kwanza la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EARTE) linalotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu Jijini  Arusha.


Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Onesho la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. FelIX John (kushoto) akiwa pamoja na mjumbe wa kamati hiyo Bi. Lilian Fungamtama (kulia) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Onesho  hilo  litakalofanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Arusha.


Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Maseke Mabiki akifuatilia Mkutano wa Waandishi  wa habari uliokuwa ukiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja wa kutoa taarifa kwa umma kuhusiana na Onesho la Kitalii la Afrika Mashariki EARTE litakalofanyika Jijini Arusha.


Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx


Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Tanzania itakuwa mwenyeji wa kwanza wa onesho la Utalii wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  (EARTE).


Lengo la onesho hilo hapa nchini ni kuvutia na kukuza uwekezaji katika sekta ya Utalii.


Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma , Mhe. Masanja amesema onesho hilo litakuwa linafanyika kwa mzunguko katika nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kila mwaka .


 "Onesho la EARTE litafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe  9 hadi 16 Oktoba, 2021 ambapo litajumuisha  siku tatu za maonesho  na siku tano za ziara maalum ya  kutembelea vivutio vya utalii pamoja na fursa za utalii  wa ndani kwa Tanzania Bara na Zanzibar," amesema  Mhe. Masanja.


Wakati huo huo ,amefafanua kuwa,  kwa kutambua Utalii kama  sekta mtambuka onesho  hilo ni fursa muhimu ya kuhamasisha uhifadhi wa Maliasili na Malikale.

0/Post a Comment/Comments