Waelimisheni wajasiliamali wajue kujitangaza kwakutumia bidhaa za korosho wanazo sindika na kufunga zikiwa kwenye viwango na ubora unaotakiwa sokoni.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Generali Marco Gaguti kwenye mafunzo ya wasindikaji na wafungaji wa bidhaa za korosho yaliyoandaliwa na shirika la Ubora wa Viwango nchini (TBS) pamoja na shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO).
Alisema kuwa ili kupata bidhaa bora wasindikaji wanapaswa kupata elimu ya mara kwa mara itakayowasaidia kuboresha bidhaa zao ili kuweza kujitangaza zikiwa na viwango sahihi.
Gaguti alisema kuwa kumekuwa na korosho nyingi zikiuzwa bila kujua zimetoka wapi zinatengenezwa na kiwanda gani zinatoka wapi?
Aidha alisema kuwa utolewaji wa elimu hiyo uendane sambamba na mpango maalum wa kuwezesha wajasiliamali hao kupata mashine kutoka SIDO ili tuweze kuongeza thamani ya korosho kwakuzibangua nchini.
Hata hivyo uwepo wa viwanda vidogo vingi unaongeza ajira kwa watanzania wengi lakini ppia inaongeza pato la taifa zaidi ya korosho ghafi.
Natamani kuona korosho zote zinazolimwa nchini zikibanguliwa hapa hapa nitapanga muda ili niweze kuwatembelea wabanguaji wote na kujifunza zaidi ili nione maandalizi lakini pia tujue ubora ukoje kuanzia shambani"
"Tujikite kwenye ubora na viwango vinavyotakiwa ili tunapotangaza korosho zetu ama zinapoliwa kokote duniani zijulikane zimetoka wapi kwa radha na ubora wa hali ya juu lakini pia hakikisheni hawa wasindikaji wote wanapata alama ya ubora mnawatemmbelea na kujua changamoto zao"
"Si vibaya kama maeneo yatatengwa ili kufahamu wanapopatikana ni zuri zaidi hii itasaidia kupewa mikopo ili kurahisisha uongezaji wa thamani wa korosho zetu" alisema Gaguti
Nae Meneja wa TBS Kanda ya kusini Amina Kitindi alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa ili kuwajengea uelewa wa katika mnyororo wa kuongeza thamani katika zao la korosho.
Alisema kuwa katika mafunzo hayo wamehidhuria maafisa kilimo, afya, watalaamu wa viwango ili kuhakikisha kuwa wanakidhi vigezo vinavyotakiwa na shirika la viwango.
"Tunatoa mafunzo haya ili kuhakikisha kuwa tunapata bidhaa bora itakayoendana na fedha anayoitumia pia italinda afya ya mtumiaji" alisema Kitindi
Nae Meneja Utafiti na mafunzo kutoka TBS Hamis Sudi alisema kuwa wasindikaji wengi wanahitaji elimu zaidi ili kuweza kufikia viwango vinavyotakiwa na shirika hilo.
"Tutawatembelea ili tuangalie nini kikwazo cha kutofikia malengo ili kuongeza wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi tunataka bidhaa zenye viwango na ubora wa kimataifa ndio maana tumejikita kwenye zao la korosho, sekta ya chakula na nyama" alisema Sudi
MWISHO

Post a Comment