TMA :MVUA ZA VULI 2021 ZINATARAJIWA KUWA CHINI YA WASTANI HADI WASTANI.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA)  Dkt Hamza Kabelwa wakati akizungumza na wanahabari akitoa mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kwa Kipindi cha Oktoba mpaka Disemba mwaka huu

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa TMA, Dk. Hamza Kabelwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari akitoa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli za Oktoba hadi Disemba 2021. Kushoto ni Meneja wa Kituo cha Huduma za Utabiri wa TMA, Samuel Mbuya 

.............................................................................. 

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM 

Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za vuli mwaka huu zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani zikiambatana na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi yanayopata mvua za vuli. 

Hayo yameelewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa  Huduma za Utabiri TMA Dkt Hamza Kabelwa wakati akizungumza na wanahabari akitoa mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli kwa Kipindi cha Oktoba mpaka Disemba mwaka huu ambapo amesema msimu huo unatarajiwa kuanza kwa kusuasua katika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Oktoba. 


Dkt Kabelwa amesema athari zinazoweza kujitokeza kipindi hicho ni pamoja na kuibuka kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na upungufu wa maji safi na salama lakini pia kusababisha upungufu wa malisho na maji hivyo kusababisha kujitokeza kwa migogoro kati ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.


‘Kanda ya Ziwa Victoria mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mngi ya mikoa ya Kagra,Gita,Mwanza,Magharib mwa mkoa wa Shinyanga pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma’amsema Dkt Kabelwa 

Aidha katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini ikijumuisha kaskazini mwa mkoa wa Morogoro,Mikoa ya Pwani,Dar es salaam,Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba mvua zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Pwani ya kaskazini. 

Akielezea Mikoa ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki ikijumuisha mikoa ya Arusha,Manyara pamoja na Kilimanjaro amesema mvua zinatarajiwa kuwa za chini ya wastani hadi wastani katika maneo mengi ambapo msimu utaanza  kwa kusuasua katika wiki ya tatu na ya nne ya mwzi Oktoba mwaka huu na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu.

Dkt Kabelwa amesema katika maeneo ambayo yanatarajiwa kupata mvua chini ya wastani hadi wastani,menejiment za maafa ni vyema zikashirikiana na kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula,malisho ya mifugo,maji na kutoa miongozo ya kukabiliana na maafa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumzia utabiri wa Ngazi za Wilaya ,Kaimu Mkurugenzi huyo amesema lengo lao ni kuhakikisha taarifa za hali ya hewa zinatumika ipasavyo katika maeneo madogo ili kuweza kuongeza tija ufanisi na kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza. 

Hata hivyo Imeelezwa kuwa Mamlaka hiyo itandelea kufuatilia mwnendo wa mifumo ya hali ya hewa na kutoa mirejesho ya mwelekeo wa Mvua nchini kadri inavyohitajika hivyo wadau wameshauriwa kupata taarifa mahususi za utabiri wa msimu ili kukidhi mahiutaji katika sekta zao. 

0/Post a Comment/Comments