UONGOZI WA MACHINGA DAR ES SALAAM WAPONGEZA KIKAO CHA RC MAKALLA KUHUSU KUWAPANGA MACHINGA





 Wasema wapo tayari kupangwa kwenye maeneo rasmi.

- *Wakiri kufanya biashara kwenye maeneo  yasiyo rasmi na kuhatarisha usalama.

- *RC Makalla asema *lengo la Serikali ni kuona biashara zinafanyika na watu wanapata kipato.*


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Amos Makalla* leo September 16 amefanya *kikao Cha pamoja na uongozi wa Machinga Mkoa wa Dar es salaam* kuhusu *njia Bora ya Kuwapanga Machinga* Jijini humo.

Katika kikao hicho *Uongozi wa Machinga* umepongeza hatua ya *RC Makalla* kutumia *njia ya shirikishi* Jambo lililotoa fursa kwa Machinga *kuwa huru* kutoa *maoni na mapendekezo* mbalimbali yenye mrengo wa *kufanikisha maelekezo ya Serikali.*

Akizungumza Katika kikao hicho *RC Makalla* amefurahi kuona *kikao hicho kimemalizika kwa Mafanikio makubwa* ambapo ameahidi *kushughulikia mapendekezo yote yaliyotolewa* kwa kushirikiana na *Wakuu wa Wilaya.*

Aidha *RC Makalla* amesema miongoni mwa *maeneo atakayoanza kuyafanyia kazi* ni pamoja na kuwapanga Machinga *waliojenga Vibanda juu ya Mitaro na mifereji,* Wanaofanya biashara Kwenye *njia za watembea kwa miguu,* wanaofanya biashara *mbele ya Maduka,* wanaofanya biashara Kwenye *hifadhi ya Barabara* na wanaofanya biashara *mbele ya Taasisi za Umma zikiwemo shule.*

Pamoja na hayo *RC Makalla* ametoa Fursa kwa Viongozi wa Machinga *kupendekeza maeneo ya Wazi wanayoona yanafaa kwa biashara* ili wapatiwe na ameahidi kuweka *mazingira Bora ya biashara* ikiwemo kufikisha *huduma ya Usafiri.*

Hata hivyo *RC Makalla* amesema Serikali itaendelea *kutoa elimu* ya kutosha Wafanyabiashara kwakuwa *lengo la Serikali ni kuona biashara zinafanyika na watu wanapata kipato.*

Kwa upande wao Viongozi wa Machinga akiwemo *Makamu Mwenyekiti* wa Machinga Bwana *Steven Lusinde* amemshukuru *RC Makalla* kwa uamuzi wa kukutana nao na *kuwasikiliza* Jambo lililowezesha *kila upande kutoa maoni na mapendekezo* ya namna Bora ya *kufanikisha Mpango huo* na Wana Imani kwa *Mpango wa kuwapanga Machinga Dar es salaam utakuwa na mafanikio makubwa.*

0/Post a Comment/Comments