UZINDUZI WA MWONGOZO WA KODI KWA ASASI ZA KIRAIA KUONGEZA MCHANGO KATIKA ULIPAJI KODI

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Feliciana Nkane (katikati) akizungumza katika hafla ya  uzinduzi wa  mwongozo wa  Kodi kwa Asasi za Kiraia (CSO Tax Tool-Kit) ambao umeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kushoto kwake ni Mratibu Kitaifa wa Mtandao THRDC Onesmo Olengurumwa na kulia ni mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa akizungumza.

Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Feliciana Nkane (katikati ) Mratibu Kitaifa wa Mtandao THRDC Onesmo Olengurumwa (kushoto) na mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo (kulia) pamoja na Jackson Mmary kutoka Taasisi ya Wajibu Institute wakati wa uzinduzi wa  mwongozo wa  Kodi kwa Asasi za Kiraia (CSO Tax Tool-Kit) 

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa akimkabidhi Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Feliciana Nkane mwongozo wa  Kodi kwa Asasi za Kiraia (CSO Tax Tool-Kit)

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) Onesmo Olengurumwa , Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Feliciana Nkane, mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo (kulia) pamoja na Jackson Mmary kutoka Taasisi ya Wajibu Institute pamoja na watendaji wa THRDC katika picha ya Pamoja baada ya  mwongozo wa  Kodi kwa Asasi za Kiraia (CSO Tax Tool-Kit)

.........................................................

NA MUSSA KHALID DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,imeahidi kushirikiana vyema na Asasi za Kiraia ili kuhakikisha AZAKI zote nchini zinapata Uelelewa wa maswala ya ulipaji kodi na utekelezaji wa sera na sheria za kodi nchini. 

Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika hafla ya  uzinduzi wa  mwongozo wa  Kodi kwa Asasi za Kiraia (CSO Tax Tool-Kit) ambao umeratibiwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Akizungumza kwa niaba ya Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Feliciana Nkane amezipongeza Asasi zote zilizoshiriki katika mchakato wa kuandaa mwongozo wa kodi kwa ajili ya asasi za kiraia na kueleza kuwa AZAKI zimekuwa na mchango mkubwa kwa mapato ambayo yamekuwa yakitumika katika uwezeshaji wa shughuli mbali mbali za kijamiii.

“Sisi kama TRA tutasambaza nakala za mwongozo huu katika ofisi zetu zote za wilaya ili ninyi AZAKI muweze kupata nakala bure pasi na malipo yoyote. Hii ni kusudi asasi nyingi zaidi zifaidike na taarifa zilizomo katika mwongozo huu ikiwemo taratibu za namna ya kuomba kibali cha hadhi va kutolipa kodi (Charitable status)”amesema Nkane

Aidha ametoa wito kwa wadau wote katika sekta ya Asasi za Kiraia kupata nakala za muongozo huo,ikiwa ni pamoja na  kutilia maanani yaliyomo, na pia kuwashirikisha na wengine katika maeneo yao.

Awali akizungumza Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC Onesmo Olengurumwa ameeleza kuwa Mwongozo huo uliozinduliwa ni nyenzo muhimu katika kukuza uelewa na utekelezaji wa sera na sheria za kodi kwa asasi za kiraia. 

Olengurumwa amesema mwongozo huo utaweza kuzisaidia Asasi za Kiraia katika maswala ya ulipaji Kodi ambayo awali yalikuwa yakifanyika kwa usumbufu mkubwa kutokana na Asasi za Kiraia kutokuwa na uelewa mpana wa mahitaji yaliyotakiwa na Mamlaka ili kutimiza wajibu wao.

“Mwongozo huu umejikita katika kuelezea maeneo ambayo yana changamoto katika ulipaji wa kodi kutoka Asasi a Kiraia ili kukuza uelewa na utekelezaji wa sera na sheria za kodi” Amesema Olengurumwa

Mratibu huyo Kitaifa wa THRDC ameendea kueleza kuwa mwongozo huo unaelezea dhana tofauti kuhusu aina tofauti za kodi ikiwa ni pamoja na ushuru na kodi mbalimbali lakini pia kwa namna gani taasisa inaweza kuwa Taasis ya Kihisani (Charitable organization) na namna taasisi za kihisani zinatozwa kodi.

Kwa upande wake Jackson Mmary kutoka Taasisi ya Wajibu Institute amesema wanaamini kwamba NGO’s zote zinajukumu la kulipa kodi hivyo kutengenezwa kwa mwongozo huo utasaidia kuwezesha taasisi zote kulipa kodi kwa ufanisi.

Hata hivyo Mratibu Kitaifa wa THRDC Olengurumwa amesema mchango wa Asasi za Kiraia (AZAKI) katika pato la taifa, umekua ni mkubwa sana, kwani AZAKI mbalimbali kutoka kote nchini zimekuwa zikichangia pato la taifa kupitia kodi mbalimbali kama vile Kodi ya Mapato (PAYE), Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Withholding Tax (Kodi ya Zuio) , Kodi ya Mhuri (Stamp Duty) na kodi zingine nyingi.

0/Post a Comment/Comments