Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akifuatilia mada mbalimbali
zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri
lililofanyika Cairo Misri.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, akifuatilia mada
mbalimbali zilizowasilishwa wakati wa Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano
la Misri lililofanyika Cairo Misri.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Balozi wa
Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali Anselm Bahati, baada
ya Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri lililofanyika Cairo
Misri.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja Jenerali
Anselm Bahati (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,
Mhe. Daniel Sillo, alipotembelea ofisi za ubalozi Cairo nchini Misri.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya
pamoja na watumishi wa ubalozi nchini Misri alipotembelea ofisi na kufanya
kikao cha ndani. Wa nne kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mhe.
Meja Jenerali Anselm Bahati na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya
Fedha na Mipango - Misri)
..........................................................
Na. Josephine Majula,
WFM – Cairo Misri
Wajumbe wa
Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt
International Cooperation Forum) ikiwemo Tanzania wamekubaliana kutoa
ripoti ya tathimini ya mkutano huo baada ya miezi mitatu ambapo yote
yaliyojadiliwa na kukubaliwa likiwemo suala la kuendeleza ukuaji wa uchumi
licha ya changamoto ya Covid 19 yatatolewa mwongozo kwa ajili ya utekelezaji.
Hayo yamebainishwa na
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa
kuhitimisha Kongamano la Kimataifa la Ushirikiano la Misri (Egypt
International Cooperation Forum) lililofanyika kwa siku mbili mjini
Cairo nchini Misri.
Dkt. Mwigulu alisema
kongamano hilo limemalizika na ajenda mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo za
mikakati ya kupambana na Uviko- 19 na umuhimu wa mahusiano ya kimataifa katika
kujijenga kiuchumi.
Katika hatua nyingine
Dkt. Mwigulu alitembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Misri ambapo
alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Misri Mhe. Meja
Jenerali Anselm Bahati.
Ujumbe wa Tanzania
uliongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba,
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Daniel Sillo, Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban na wataalamu
kutoka wizara hiyo.
MWISHO.
Post a Comment