
Wananchi
wa Kata ya Keko Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam wakiwa wamesimama nje
ya geti la Kampuni ya REDSEA CO.LTD ili kupata muafaka wa mgogoro wamfereji wa
maji unaopita katika maeneo yao

Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave alipokuwa akishuhudia mfereji huo
Mfereji
wa maji machafu unaodwaiwa kuzibwa na Kampuni ya REDSEA CO.LTD na kusababisha
kukumbwa na mafuriko ya maji machafu
Diwani wa Kata ya Keko Jasdeep Singh Babhra akizungumza na mwandishi wa habari hizi
.................................................................
NA
MUSSA KHALID ,DAR ES SALAAM
Wananchi
wa Kata ya Keko Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam wameilalamikia serikali
kwa kutowatatulia changamoto ya mfereji wa maji ambao unadaiwa kuzibwa na
Kampuni ya REDSEA CO.LTD na kusababisha kukumbwa na mafuriko ya maji machafu.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es salaam wananchi hao ambao wamejikusanya pembezoni
mwa kampuni hiyo na kutoa kero zao mbele ya Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave wamesema
kutokana na kutoboreshwa kwa mfereji huo ambao umejengwa eneo la Azania umesababisha
wakumbane na adha hasa nyakati za mvua.
Wamesema ujenzi wa mfereji
huo umeanza kujengwa kwa muda mrefu na haujawekwa mwendelezo wa maji kwenda baharini hivyo kusababisha kujaa maji na kuingia katika makazi ya watu.
Akizungumzia Changamoto hiyo
Mbunge wa Jimbo la Temeke Dorothy Kilave amesema baada ya kukutana na Uongozi
wa Kampuni hiyo wameazimia kupewa maelezo ya kibali cha kujenga mfereji huo
ambacho wamepewa na Manispaa kama wanavyodai ili waweze kupitia na kisha
kuchukua hatua.
Kwa upande wake Kaimu Meneja
wa TARURA Temeke Mhandisi Kweyamba Adelhard amesema watafanya upembuzi wa
kibali ambacho kampuni hiyo imeomba cha kujenga mfereji huo na kama imekiuka
masharti watamrudisha Manispaa na kukifuta kibali hicho.
Naye Diwani wa Kata ya Keko Jasdeep
Singh Babhra amesema wanaendelea kufuatilia na hivyo amewataka wananchi kuwa
watulivu kwani yeye ni mwakilishi wao hivyo atahakikisha linatatulika.
Diwani huo amesema Mfereji huo sio wa Wilaya bali ni waKitaifa hivyo baada ya kufika kwa Mbunge pia atalifikisha Mpaka kwa waziri wa Ujenzi pamoja na TAMISEMI ili changamoto hiyo iweze kutatulika .

Post a Comment