WANAOPANGISHA MAGOMENI KOTA NI MATAPELI:RC MAKALLA







Asema Serikali inawatambua Kaya 644 zilizokuwepo awali.




Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam  Amos Makalla amezihakikishia Kaya zote 644 wakazi wa Magomeni Kota kuwa   Serikali itawapatia Makazi watu wote wanaostahili na walioainishwa tokea awali ambapo amewataka kuwapuuza wote wanaosambaza taarifa za uvumi.

Akizungumza leo wakati alipofanya ziara ya Kujiridhisha na kukagua maendeleo ya Mradi huo Wenye thamani ya Shilingi bilioni 52.1 ambapo kwa Sasa Ujenzi umefikia 99% na ukikamilika utanufaisha Watu zaidi ya 3,000 kutoka Kaya 644 na sasa TANESCO wapo kwenye hatua za kuweka miundombinu ya umeme.


Aidha RC Makalla amesema Mradi utakapokamilika Wakazi husika wataitwa na kutangaziwa tarehe rasmi ya kuingia Katika nyumba hizo hivyo wawe watulivu.

Hata hivyo RC Makalla ametoa wito kwa Wakala wa Majengo TBA kutumia eneo lililobaki kimkakati kwa kujenga Majengo ya Gorofa ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa Ardhi.


Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi yake ya kusimamia na kukamilisha miradi yote ya maendeleo na hii inajirihidhisha kupitia Mradi wa Magomeni Kota.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya miliki Said Mndeme amesema, hadi sasa makazi yao yamekamilika na mchakato uliopo ni wa kuingiza umeme na tayari transfoma tano zimefungwa na zoezi hilo litakapokamilika hatua itakayofuata na kutoa semina elekezi kwa wapangaji 644 watakaoingia katika nyumba hizo.

Mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi ya waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota ulianza October mosi 2016 ukihusisha Ujenzi wa Majengo matano yenye Gorofa nane Hadi Tisa ambapo ukikamilika wanufaika wataishi Bure ndani ya Nyumba hizo kwa kipindi Cha miaka mitano


0/Post a Comment/Comments