Muhudumu Pekee Wa Zahanati Ya
Nambunju Rehema Saidi Mhimbwa
NA SALIM BITCHUKA
Wakazi wa kijiji cha Nambunju Kata Mbwara
tarafa ya Mohoro wilaya ya Rufiji
mkoani Pwani wameiomba Serikali kuwaongezea
Wahudumu wa Afya Katika Zahanati iliyopo
kijijini hapo.
Wakizungumza na kituo hiki kutoka mkoani
Pwani wakazi hao wamesema katika Zahanati
hiyo kumekuwa ma muhudumu mmoja kitendo
kinachopelekea kukosekana ufanisi wa kazi na
kuhatarisha maisha ya wakazi wa kijiji
cha Nambunju hasa pale kunapokuwepo
wagonjwa wengi kwa wakati mmoja katika
kituo hicho cha Afya.
Aidha kwa upande wake muhudumu pekee
wa Zahanati ya Nambunju Rehema Saidi Mhimbwa
amekiri kuwa ni yeye pekee anayehudumia
katika kituo hicho kwa zaidi ya miezi
ya miezi Mitano huku akisema kuwa
changamoto kubwa ni wingi wa watu
wanaohitaji huduma na pale anapopatwa na
dharura hupelekea kufunga kituo.
Mbali na uhaba wa watoa huduma
katika kituo hicho cha Afya , kijiji
cha Nambunju Mkoani Pwani kinakabiliwa na
kero nyingi ikiwemo ubovu wa barabara ,
ukosefu wa usafiri wa kutosha , ukosefu wa
Maji safi na Salama , vyumba vya madarasa
,madawati, ukosefu wa mawasiliano ya simu ya
uhakika kitendo kinachowaibua
wananchi kutaka viongozi wa ngazi za juu
wa Serikali kutembelea Kijijini hapo.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa
Kijiji cha Nambunju Maliki Hamidi
pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji
Abdallah Hemedi Kipuli kwa pamoja wamekiri
uwepo wa matatizo hayo huku wakisema kuwa
baadhi ya matatizo tayari
yamewasilishwa katika ngazi husika ikiwemo
ubovu wa barabara pamoja uhaba wa
watoa huduma katika Zahanati ya Nambunju.
Post a Comment