******************************************
Na Mwandishi wetuSHINDANO la Ma Dj linaloandaliwa na Castle lite unlocks imezindua Superior sets tour ya kimuziki itakayopitia na kutembelea miji 7 na kushirikisha Ma Dj 7 wa kimataifa kutoka Afrika Karebiani pamoja na Ma Dj 7 kutoka nyumbani Tanzania
Akizungumza na waandishi wa habari Brand Meneja wa Castle lite katika siku ya uvumbuzi, Silvanus Mazula amesema watakaocheza muziki kwa timu za Ma Dj wawili wawili kuanzia Novemba mwaka huu huko Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza, Kahama, Mbeya na Dar es Salaam.
"Tunaanzisha mfululizo wa matukio kwa namna ambayo haijawahi kutokea hapo awali, kama ambavyo Castle lite Unlocks inawaleta pamoja na wasanii wa ndani na wakimataifa na wanyumbani katika namna mpya, bora Maya hadhi ya juuzaidi" amesema Mzula
Aidha Dj wa kimataifawaliochaguliwa ni Dj Vjeezy, (Zambia) Dj Creme, (Kenya) Dj Bryan (Uganda) Dj Musa Keys (Afrika Kusini) Dj Commissioner Wysei, (Nigeria) Dj Alba Nalo (Namibia) na Dj Puffy (Barbados)
Wananchi watapiga kura kubaini ni ma Dj gani kutoka nchini Tanzania watakaoshiriki kutoka kwenye orodha ya Ma Dj maarufu nchini Tanzania.
Post a Comment