NA SIXMUND J. BEGASHE
Wazazi nchini wametakiwa
kuwarithisha watoto wao urithi wa kiutamaduni wa asili ya makabila yao ili
kujenga kizazi kinacho tambua asili yake na hasa misingi ya Utanzania
iliyojengwa kwa mila na desturi za Makabila ya hapa nchini badala ya kuwaachia
wakatekwa na tamaduni za kigeni.
Wito huo umetolewa na
Mkurugenzi wa Utamaduni nchini Dkt Emmanuel Temu, aliemwakilisha Waziri wa
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa (MB) kwenye siku ya utamaduni
iliyo andaliwa na Shule ya Awali na Msingi ya Mt JOSEFU
iliyopo Mbezi Beach Dar es Salaam
Dkt Temu zaidi ya kuto
pongezi kwa shule ya Awali na Msingi ya Mt Josefu, amesema Serikali itaendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali wa Utamaduni ili kuhakikisha dhima ya
nchi ya kuwa na kizazi kinacho thamini utamaduni wake inaendelea na kufikiwa
kwa kiwango kikubwa zaidi, hivyo amezitaka shule hapa nchini kuhakikisha
zinakuwa na program elimishi juu ya utamaduni wa Mtanzania.
Mkurugenzi wa Shule ya Awali
na Msingi ya Mt Josefu Bi Christa Pendo Rweyemamu amesema kuna
licha ya shule yao kufundisha kwa lugha ya kingereza lakini wameona umuhimu wa
kuwa na siku ya utamaduni katika shule hiyo kwa kushirikisha wazazi, jamii
inayowazuguka na taifa kwa ujumla kwa sababu wazazi walio wengi siku hizi hawapati muda wa kuendeleza asili na
tamaduni za kwao hivyo kupelekea watoto wengi kutofahamu, kusahau au kutojua
kabisa asili yao ambayo inabeba misingi ya utu, uzalendo na utanzania wetu.
“Ni
wazi hali hiyo ikiachwa inaweza kuhatarisha utambulisho wetu kama watanzania.
Hivi leo kutokana na utandawazi, watoto wetu wanajua zaidi kuhusu tamaduni za
mataifa mengine kuliko za kwao. Leo hii televisheni, redio na mitandao imejaa
filamu na miziki ya Ulaya na Marekan. Wenzetu walitushinda kwa kuwa tamaduni
zao zimenakiliwa kwa kina na kuchapishwa maradufu”. Aliongeza Bi Rweyemamu
Afisa Elimu Mwandamizi wa
Makumbusho ya Taifa Bi Alhelmina Joseph licha ya kuupongeza ongozi wa shule
hiyo kwa kushirikiana kwa karibu na Makumbusho ya Taifa nchini katika kuwaelimisha
watoto na walimu mambo muhimu yanayohusu Utamaduni, ametoa wito kwa Shule na
taasisi zingine kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha uhifadhi wa
urithi wa kiutamaduni nchini unakuwa endelevu.
“Kwa kweli shule hii ya Awali na Msingi Mt Josefu hapa Mbezi Beach
inastahili pongezi za dhati kabisa, wamekuwa wakishirikiana nasi kwa muda mrefu
sasa, kwetu ni wadau muhimu sana katika uhifadhi wa urithi wa Utamaduni,
tumejionea hapa watoto wakijifunza mapishi, kuvaa kiasili, nyumba za asili, ngoma
za asili na mambomengi, hakika hii haitasahaulika kwa wote tuliofika
hapa.” Alisema Bi Joseph
Mwanafunzi wa shule hiyo,
victor Chales na Zuhura Fadhili wamesema licha ya burudani waliyoipata kupitia
maonesho hayo pia wameweza kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu makabila yao
pamoja na ya watoto wengine jambo linalo wapa ufahamu zaidi juu ya utajiri
mkubwa wa urithi wa utamaduni uliopo nchini.
Akielezea umuhimu wa mafunzo
hayo ya utamaduni, Mwana wa Mfalme wa Pili wa Kabila la Wahaya Mlangira Katega
wapili ameishari serikali kuhakikisha kuanzisha mitaala ya somo la Utamaduni
mashuleni ili shule zote nchini zinawafundisha watoto Utamaduni wa Mtanzania
ambao upo mbioni kutoweka
“Utamaduni wa kijadi yaani wa kirohoo, ni muhimu sana, hata Rais wetu Mama
Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni HANGAI wetu alisema watalii wanakuja wanakaa
sikumoja mbili kwa sababu hakuna mambo mengi ya kuona, lakini wakizunguka
tunakabila zaidi ya 120, vyakula, ngoma mbalimbali kama tunavyoona leo hapa,
mtalii anaweza kukaa mwezi, hivyo nazi kuupongeza uongozi wa shule hii kwa
jambo hili kubwa”. Malangira Katego wa Pili
Katika tamasha hili makabila
yalishindanishwa kikanda za Kaskazini, Kati, Kusini, Pwani na ya Ziwa katika
vipengele mbalimbali kama vile Utawala, Mapishi, mavazi na Kucheza ngoma ambapo
ambapo kianda ya Kaskazini ikiibuka msindi wa Jumla baada ya kushinda kipengele
cha Mapishi na Mavazi huku Pwani wakishika nafasi ya Pili baada ya kushinda
katika Ngoma.
Post a Comment